habari

Omba Omba Kuanza Kusakwa Na Kuswekwa Ndani.

on

Serikali ya Kigali nchini Rwanda imetangaza kuwawinda vikali na kuwaweka gerezani walemavu wote wanaojihusisha na vitendo vya kuomba omba barabarani Kwa madai kuwa ni chanzo cha uchafu mjini hapo uamuzi ambao umepokelewa kwa shingo upande miongoni mwa walemavu, huku baadhi ya raia wakisema kwamba uamuzi huo umekuja kwa lengo la kukandamiza walemavu na watu maskini..

Uamuzi huo ambao unaweza kutekelezwa wakati wowete kuanzia sasa umewaonya walemavu hao kuwa kama hawatositisha shughuli uombaji, watatiwa ndani.

Kwa upande mwingine, mashirika ya kiraia nchini Rwanda yameshauri kwamba, kabla ya utekelezaji hatua hiyo kufanywa kungekuwepo kwanza mazungumzo ya pande zote.

Licha ya hatua hiyo kuzua minong’ono miongoni mwa wakazi wa jiji hilo, polisi ya Rwanda imedai kama mji wa Kigali utaomba msaada, wako tayari kutekeleza kazi yao ipaswavyo kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi mjini Kigali Hitayesu Emmanuel.

Ripoti mbalimbali mbalimbali zimekuwa zikiitaja Kigali kuwa miongoni mwa miji safi barani afrika huku ripoti zingine hususani zile za kutetea haki za binadamu, zikiishutumu Kigali kwa kuwafunga watu wasiojiweza.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *