siasa

Polepole: Zitto Amekuwa Akifanya Vikao Vya Kamati Kuu Ya ACT-Wazalendo Mtandaoni.

on

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kiongozi mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amekuwa akiendesha vikao vikuu vya chama chake kupitia mitandao ya Kijamii.

‘’Siku hizi, hata vikao vya kamati kuu ya ACT-Wazalendo, Zitto amekuwa akivifanyia mtandaoni, na kuhoji inakuwaje kikao kikubwa kama hicho kinaandaliwa mtandaoni tena kupitia facebook” amesema Polepole.

Ameongezea ACT-Wazalendo kimekwisha kimebakia kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo wa Facebook na kwamba hivi karibuni wanachama wake kutoka mikoa miwili waliomba kujiunga  na CCM.

‘’Ukweli nawaambia isingekuwa huruma ningekuwa nimeshawafagia wote, yaani wote, lakini tukasema tumuache angalau ana watu kadhaa ili chama kionekane kina uhalali wa kuendelea kuwa kwenye daftari la Msajili wa Vyama vya siasa’’amesema Polepole.

Polepole amezungumza hayo pindi akiwapokea wanachama wapya 360 wakiwemo waliohama vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo na kujiunga CCM jijini Mbeya.

Aidha Polepole amewashukuru wanachama hao wapya kwa uamuzi waliouchukua kujiunga na Chama sahihi CCM.

Dar24.com

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *