habari

Polisi Ufaransa Wazuia Maandamano Ya Wanafunzi.

on

Polisi wa kukabiliana na vujo mjini Paris Ufaransa wamewaondoa wanafunzi waliokuwa wakitaka kuingia katika chuo kikuu cha Sorbonne mjini humo kama sehemu ya awamu nyingine ya maandamano ya kupinga mageuzi ya rais Emannuel Macron.

Chuo hicho kilitangaza kwamba eneo lake maarufu linalofahamika kama ukingo wa kushoto, ambalo ni chimbuko la maandamano ya wanafunzi waliokuwa na mtizamo wa siasa mrengo wa kushoto mwaka 1968 limefungwa hii leo kutokana na sababu za kiusalama baada ya kufanyika operesheni ya polisi jana alhamisi. Wakati kiasi wanafunzi 200 wakihamishwa eneo hilo mamia kadhaa wengine walikusanyika nje ya chuo wakipiga kelele za kuonesha hasira dhidi ya polisi. Hata hivyo tukio hilo lilimalizika bila ya kuzuka vurugu.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *