habari

Polisi Z’bar yamnasa mtuhumiwa wa dawa za kulevya na kete 23

on

Mohamed Khamis

Mapambano dhidi ya dawa za kulevya kisiwani Zanzibar yanaendelea kushika kasi baada jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja kufanikiwa kumtia mbaroni  Ali Juma Faki (47) mkaazi wa Kiwengwa akiwa na kete 23 zinazodaiwa kuwa za dawa za kulevya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mussa Ali Mussa, alisema tukio hilo lilitokea Aprili 13 mwaka saa 9:15 jioni  Kiwengwa Mafarasi wilaya ya kaskazini’ B’.

Alisema kijana huyo alikamatwa wakati polisi walipokuwa katika doria zao za kawaida zenye lengo la kupambana na matukio mbali mbali ya kihalifu.

Alisema wakati askari wakiwa kwenye doria katika maeneo hayo walimkuta mtuhumiwa huyo  na kumtilia mashaka ndipo walipompekuwa na kumkuta na kiwango hicho cha dawa.

Alisema mtuhumiwa huyo atapelekwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.

Hata hivyo, aliwatahadharisha wananchi kutojihusisha na biashara hizo kwani zinatia doa nchi na kuharibu vijana.

 

 

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *