habari

Raia wa Misri akamatwa Z’bar akitaka kusafirisha kobe 47

on

Na Muhamed Khamis

Unguja.Maafisa ulizi  wa mamalaka ya uwanja wa ndege Unguja wamefanikiwa kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi raia mmoja  wa Misri kwa tuhuma za kutaka kuondoka nchini akiwa na vikobe 47

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari afisa uhusiano wa mamlaka  hio Mulhat Yussuf Said alimtaha  raia huyo wa Egypt kuwa ni Mohamed Abdul/hamim m Tolba (33)

Amesema raia huyo wa kigeni alipanga kusafiri jana tarehe 14 majira ya alaasiri kwa ndege ya Ethiopia ET 814 na kwamba maafisa wa ulinzi wa mamlaka hio waliweza kubaini vikobe hivyo hivikiwa kwenye moja ya mizigo ya abiria huyo.

Akieleza baadhi ya hatua walizozichukua mara baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo amesema waliweza kumfikisha kituo cha polisi kwa ajili ya uchukuliwaji wa hatua nyengine zaidi za kisheria.

Hata hivyo amewaonya  wale wote wenye tabia hio na nyengine mbaya kwamba mamlaka ya uwanja wa ndege haitasita kumchukulia  hatua mtu yoyote yule atakaebainika kufanya vitendo visivyo faa kwa kitumia uwanja huo.

Aidha amesema watahakikisha wanaendelea kusimamia hali ya ulinzi na usalama muda wote kwenye uwanja huo kwa lengo la kuhakikisha kuinamarika kiusalama na kuondoa changamoto kwa wasafiri mbali mbali wanaotumia uwanja huo kuelekea maeneo tofauti ulwenguni.

 

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *