habari

Raia Wa Sudan Kusini Waishio Marekani Waandamana Kupinga Vita Nchini Mwao.

on

Makumi ya waandamanaji wa Sudan Kusini na wanaharakati wa kisiasa baadhi yao wakiwa ni wafuasi wa chama cha upinzani cha SPLM-IO walikusanyika mbele ya White House siku ya Jumatatu wakipinga kuendelea kwa vita katika nchi yao ya asili.

Takriban waandamanaji 25 walipiga kelele wakisema “Watu wa Sudan Kusini wanakufa” na “tunahitaji amani nchini Sudan Kusini”.

Mwandamanaji kutoka Tennessee Elizabeth James akiongea kwa lugha ya kiarabu, alisema muda unakwenda wa kuchukua hatua kwa Sudan Kusini. “Tukiacha huu mpango wa kutafuta amani uwe kwenye mikono ya serikali na waasi,’ alisema. ‘Watachukua muda wao kwa sababu ya maslahi yao binafsi”.

James aliendesha gari kwa saa tisa kuhakikisha anashiriki maandamano ya Jumatatu akisema ilikuwa ni wajibu wake kutoa sauti kuelezea wasi wasi wake. “Wako wapi raia wa Sudan Kusini? Kila siku tunafariki, kila siku tuna njaa, kila siku tumetawanyika, kila siku tunakwenda katika nchi nyingine” James alisema.

Waandamanaji walishika mabango na kuvaa mashati yaliyoandikwa “Rais Trump ataifanya Sudan Kusini iwe nzuri tena” wakati mabango mengine yalilenga biashara ya Afrika, Mamlaka ya Maendeleo ya Kikanda-IGAD bango lililosomeka “IGAD imeshindwa na imejaa rushwa kiasi cha kushindwa kuleta amani Sudan Kusini”.

Isaac Gang, mwakilishi wa chama cha upinzani nchini Marekani na muaandaaji wa maandamano, alisema IGAD ina fursa ya kubadili mambo wakati wakiandaa mazungumzo yajayo ya amani. “Kwa kweli naamini kama wadau nchini Sudan Kusini watachukua fursa ya kufufua mkutano wa ngazi ya juu kuna jambo zuri linaweza kutokea” alisema Gang. “Lakini kama tukirejea kwenye usingizi wa kawaida watu watatumia fursa kama hii kupoteza muda kinyume na kutumia fursa kama hii kuleta Amani”.

Mazungumzo yanatarajiwa kufanyika katika wiki chache zijazo kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *