habari

Rais JPM Achangia Milion 3 Za Ujenzi Wa Vyoo Shuleni.

on

Rais John Pombe Magufuli Jumamosi hii Mei 5 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro amechangia kiasi cha pesa shilingi milioni 3 kwa shule ya Sekondari Mang’ula kwa ajili ya ujenzi wa choo.

Rais Magufuli amemsimamisha mwanafunzi mmoja wa shule ya Mang’ula na kumkabidhi kiasi hicho cha pesa mara baada ya mwanafunzi huyo wa kidato cha kwanza kuwasilisha tatizo hilo la choo kwa Rais Magufuli.

Aidha Rais amewataka wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo kuchangia kiasi kilichobaki kuhakikisha ujenzi wa choo katika shule hiyo unakamilika, amesema ujenzi ukikamilika atatembelea ili kukagua vyoo hivyo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *