siasa

Rais Maduro Atangazwa Kuwa Mshindi Katika Nafasi Ya Urais.

on

Tume ya uchaguzi nchini Venezuela, imemtangaza Rais Nicolas Maduro, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika jana Jumapili nchini humo. Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake nje ya ikulu yake mjini Caracas kufuatia ushindi huo, Rais Maduro ameusifia akiutaja kuwa wa ‘kihistoria’.

Hata hivyo upinzani umeupinga uchaguzi huo ukisema si halali na wametaka uchaguzi mpya uandaliwe baadaye mwaka huu. Mpinzani mkuu wa Maduro, Henri Falcon, amewaambia waandishi wa habari kwamba mchakato mzima wa uchaguzi ulikuwa batili. Katika taifa hilo linalokumbwa na mzozo mbaya wa uchumi, asilimia 46 ya wapiga kura pekee ndio walijitokeza kupiga kura.

Upinzani uliususia uchaguzi huo. Jumuiya ya kimataifa pia imeukosoa uchaguzi huo, ambao sasa unampa Maduro nafasi ya kutawala kwa muhula wa pili hadi mwaka 2025

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *