habari

Rais Museveni Sasa Ruksa Kugombea Tena 2021.

on

Mahakama ya katiba nchini Uganda imeidhinisha mageuzi ya katiba yaliondoa kikomo kwa umri wa kugombea urais.

Majaji wanne kati ya watano wa jopo la majaji wamesema mageuzi hayo hayakiuki katiba, na pia hayendi kinyume na muongozo wa bunge nchini.

Awali umri wa mwisho kwa kugombea ilikuwa miaka 75.

Hii ina maana Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni atakua huru kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Kikao cha kutoa uamuzi huo uliowasilishwa katika mahakama kuu huko Mbale kilianza kwa naibu jaji mkuu, Alfonse Owiny-Dollo, kuanza kwa kuomba radhi kwa mahakama kuchelewa kuanza kwa muda uliopangwa awali.

Hata hivyo mahakama imekataa kuongeza miaka ya wabunge waliotaka kusalia madarakani kwa miaka 7 badala ya mitano ya sasa.

Katika uamuzi wake Jaji Cheborion Barishaki ameeleza kwamba kuongezwa kwa muhula wa kuhudumu bunge kutoka miaka mitano hadi miaka saba itakuwani hatua ya kibinfasi na inakwenda kinyume na maadili ya uongozi bora.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *