habari

Rais Ramaphosa Akabiliana Na Maandamano.

on

Polisi nchini Afrika Kusini ilirazimika kutumia risasi za mpira pamoja na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu wa Mahikeng wa jimbo la Kaskazini Magharibi jana ijumaa, huku Rais Cyril Pamaphosa akiwasili katika eneo na kujaribu kutuliza machafuko hayo.

Ramaphosa alilazimika kufupisha siku ziara yake ya nchini Uingereza alipokuwa anahudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola na kurudi Afrika Kusini kuja kushikamana na wenzake wa chama tawala cha African National Congress (ANC) na kisha kukutana na viongozi wa jamii. Maandamano hayo ni changamoto kwa Ramaphosa alieingia madarakani kama rais mwezi Febuari baada ya kumpokea Jacob Zuma.

Na DW.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *