siasa

Rais Wa Nigeria Kuwania Tena Urais 2019.

on

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari wiki hii alithibitisha kuwa atawania tena urais kwa muhula wa pili mwaka 2019. Hatua hii inamaliza uvumi wa muda mrefu kuhusu hatima ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 ambaye amekuwa akisumbuliwa na afya mara kwa mara.

Buhari atawasilisha ombi kwa chama chake APC, kuomba tiketi ya chama hicho kuelekea Uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Februari mwakani.

Mwanasiasa huyo  Mwislamu kutoka Kaskazini kwa Nigeria alikuwa mwanasiasa wa kwanza wa upinzani kumshinda rais aliye madarakani wakati huo Goodluck Jonathan.

Hatima yake sasa ipo mikononi mwa chama chake ambacho kitakutana kuamua iwapo atawania tena wadhifa huo licha ya umri wake mkubwa na hali yake ya kiafya.

Buhari ambaye mara kwa mara amekuwa akizuru nchini Uingereza kupata matibabu, uongozi wake umekuwa ikipambana na ufisadi na kuimarisha uchumi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *