habari

RC OTHAMAN AWATOA HOFU WAANANCHI WA KISIWA CHA UVINJE WILAYA YA WETE PEMBA

on

IMG_4141

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

NA MASANJA MABULA -PEMBA

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba mhe Omar Khamis Othman amewatoa hofu wananchi wa kisiwa cha Uvinje kilichopo wilaya ya Wete kwamba  mila na tamaduni zao , zitaendelea kudumishwa na mwekezaji ambaye anatarajia kuwekeza hoteli ya kitalii ya nyota sita katika kisiwa hicho.

 Amesema kuwa dhana ya kwamba mila na tamaduni zao zitavunjwa na mwekezaji huyo sio sahihi kwani mwekezaji huyo atafuata na kuheshimu tamadunina mila za wenyeji wa kisiwa hicho.

Akizungumza  na wananchi wa kisiwa hicho, mhe omar  amewataka kushirikiana na mwekezaji huyo ambaye amekusudia kukuza kipato chao na Taifa kwa ujumla.

“Hii ni fursa imetokea katika kisiwa hichi, changamkieni kwani kila ambaye atakuwa tayari kufanya kazi atajipatia ajira, na mzungu hawezi kukulipa kwa kipita kwenye eneo lake ni lazima ufanye kazi”alifahamisha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali amesema serikali imejipanga kuhakikisha kwamba Utalii hauleti madhara kwa wananchi.

Ameeleza kuwa serikali ya Mkoa na wilaya itaweka makubaliano na mwekezaji huyo na haitakuwa tayari kuona makubali hayo yanakiukwa.

“Tutaweka makubaliano kati ya serikali na mwekezaji, na mimi sitakuwa tayari kuona makubaliano hayo yanakiukwa na upande mmoja , na kwamba nitakuwa na utaratibu wa kufuatilia makubaliano hayo”alieleza.

 Mwakilishi wa mwekezaji huyo Fransisco Camelingo amewataka wakaazi wa kisiwa hicho hususani wenye fani za ujenzi na  wafanyabiashara , kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kuuza bidhaa zao.

Amesema kwamba atafurahi sana kufanya kazi na wenyeji wa kisiwa hicho , ambapo wenyeji watapewa kipaumbele cha kwanza.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Sharif Ali amesema tamko la serikali la kusimamia udhibiti wa maadili na tamaduni , amelipokea kwa mkono mmoja.

 “Mimi binafsi nimefarajika sana kusikia serikali itasiamamia ili kudhibiti maadili na tamaduni zetu, hivyo naaunga mkono kwa asilimia zote , naahidi kuwaelimisha ili tuweze kushiirikiana na serikali yetu kuleta maendeleo”alisema.

Hata hivyo amesema ni vyema serikali kuwa karibu na wakaazi wa kisiwa hicho ili kuwaelimisha umuhimu wa sekta ya utalii katika kuchangia maendeleo ya nchi na wananchi wake.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *