habari

RPC Lazaro Mambosasa Asema waliomteka mfanya biashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili

on

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji
Mambosasa amesema kwamba wameweka vizuizi  kila sehemu kuhakikisha hakuna mtu anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi, na kwamba waliohusika kwenye tukio la kumteka  ni raia wawili wa kigeni.

Amesema hadi sasa watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio hilo.

Mohammed Dewji, anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto leo saa 11 Alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi Gym ya Colosseum, Oysterbay Dar es salaam.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *