michezo

Salah Apewa Tuzo Ya Mchezaji Bora EPL Mwezi March.

on

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England kwa mwezi Machi baada ya kuendelea kufanya kazi nzuri katika klabu hiyo.

Hii inakuwa nara ya tatu kwa msimu huu pekee nyota huyo wa Misri huyo kutwaa tuzo hiyo, baada ya kuchukua miezi ya Novemba mwaka jana na Februari, mwaka huu.

Tangu amerejea England msimu huu akijiunga na Liverpool, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaonekana mchezaji mwenye kiwango cha juu.
Salah amevunja rekodi ya Didier Drogba ya mchezaji kutoka Afrika kufunga mabao mengi kwa msimu baada ya kufunga bao la ushindi dakika za lala salaam, Uwanja wa  Selhurst Park dhidi Crystal Palace.

Naye kocha wa Burnley, Sean Dyche ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Machi, wakati Jamie Vardy wa Leicester City ameshinda tuzo ya Bao Bora la Mwezi Machi.
Dyche ameiwezesha Burnley kushinda mechi zake zote za mwezi akianza na Everton, West Ham na West Brom, wakati Jamie Vardy ametwaa tuzo hiyo baada ya vao lake zuri alilofunga dhidi ya West Bromkwch Albion kwenye ushindj wa 4-1 Machi 10.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *