habari

Serikali Ya DRC Yakubali Kujibu Madai Ya Madaktari.

on

Kamati ya kitaifa inayotetea maslahi ya madaktari wa DR Congo (SYMECO) imetangaza kuwa mgomo uliokuwa umepangwa kufanyika Jumatatu hii Aprili 30 katika nchi nzima hautafanyika tena.

Juvenal Muanda Nlenda Mkuu wa Kamati hiyo, amesema serikali imekubali kujibu madai yao, ambayo ni ongezeko la mshara kwa asilimia 100 miongoni mwa madai mengine.

Madaktari nchini DR Congo walikua wanaomba serikali kuboresha mishahara yao, huku wakiishutumu kutoheshimu makubaliano walioafikiana mwaka jana kuhusu madai yao.

Madaktari waliku wanadai kupewa mshahara mzuri, malipo ya kazi zao za ziada, kutambuliwa kwa vyeo vyao na ufumbuzi kwa madaktari mia moja waliyofukuzwa kinyume cha sheria mwaka 2016 kwa mujibu wa madaktari hao, na ambao hufanya kazi tangu wakati huo bila malipo.

Jambo muhimu zaidi, madaktari walikua wanalalamikia ni makubaliano ya hivi karibuni yaliyosainiwa mnamo Septemba 2017 na yangelipaswa kutatua masuala yote hayo yanayozua utata. Kwa mujibu wa madaktari makubaliano hayo hayajawahi kutekelezwa.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *