habari

Shambulio La Kigaidi Laua Watatu Ubelgiji.

on

Taarifa za awali zinasema Watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Liege, nchini Ubelgiji. Katika tukio hilo Askari wawili na mwanamke wameuawa na mtu mwenye silaha ambaye pia alimshikilia mateka mtu mmoja kabla ya kuuawa na vikosi vya usalama.

Tukio hilo lilitokea saa 10:30 asubuhi (saa za Ubelhiji) kwenye barabara kuu ya Avroy ambapo Mshambuliaji alifyatua risasi kwenye umati wa watu, kabla ya kukimbilia katika shule moja la sekondari.

Wakati huo watu kadhaa walitekwa nyara, kabla ya vikosi vya usalama kuingilia kati na kufaulu kumua mshambuliaji.

Uchunguzi unaendeshwa na ofisi ya mashitaka, ambayo itachunguza kama kitendo hicho kilikua cha kigaidi.

Mwanamke aliyeuawa alikua akipita na gari lake wakati wa tukio hilo, bila hata hivyo kujua. Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya mashitaka ya Liège Catherine Collignon amesema bado uchunguzi haujatoa matokeo yoyote.

Naye  Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ubelgiji Jan Jambon amesema anasikitishwa na mauaji hayo huku akiomba raia kuwa wa tulivu, wakati uchunguzi ukiendelea.

Ubelgiji ilikumbwa na kadhia ya mauaji ya kigaidi mnamo mwezi Machi 2016, ambapo watu 32 waliuawa katika mashambulizi ya kigaidi. Tangu wakati huo nchi hiyo imeendelea kukabiliwa na mashambulizi kadhaa dhidi ya askari na maafisa wa polisi. Shambulizi la hivi karibuni lililoelezwa kuwa la kigaidi lilitokea tarehe 25 Agosti 2017 ni lile la kisu dhidi ya askari mjini Brussels.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *