habari

Shambulizi Latokea Ofisi Za Makao Makuu Ya YouTube.

on

Mtuhumiwa wa kike ameshambulia makao makuu ya ofisi za mtandao wa YouTube mjini San Bruno, karibu na San Francisco. Taarifa kutoka kwa maafisa wa Polisi pamoja na mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanamke huyo aliwajeruhi takribani watu watatu kabla ya kujiua kwa kujipiga risasi.

Mkuu wa polisi wa San Bruno, Ed Barberini amesema polisi waliwagundua watu wanne wakiwa na majeraha ya risasi wakati walipoingia kwenye ofisi za YouTube. Pia walimkuta mtu mmoja amekufa baada ya kujipiga risasi mwenyewe.

mkuu huyo amesema polisi wanaamini kuwa mtu huyo aliyejiua ndiyo mshambuliaji. Amebainisha kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba vikosi vya usalama bado vinalikagua jengo hilo. Google ambayo inaumiliki mtandao huo wa YouTube, imesema inashirikiana kwa karibu na polisi. Ikulu ya Marekani, White House imesema Rais Donald Trump amepewa taarifa na kwamba serikali yake inafuatilia hali inavyoendelea San Bruno.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *