michezo

Shangwe Za Uzinduzi Wa Copa Umisseta Zanzibar

on

Mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta, yalizinduliwa Zanzibar kwa shamrashamra mbalimbali za michezo na burudani katika uwanja wa Aman na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali,wadau wa michezo na wanafunzi wa shule za sekondari na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alisema suala la michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa inaamini kuwa inayo faida nyingi baadhi yake ikiwa ni kujenga afya, kuleta umoja, burudani na inazo fursa kubwa za ajira hususani kwa vijana na aliipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwa mstari wa mbele kudhamini mashindano haya.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Ayoub Mohamed Mahmod alipokea zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi kutoka Coca-Cola baada ya hafla ya uzinduzi.
Pia alikabidhi jezi na mpira kwa mwalimu Mussa Abdi Khamis wa shule ya sekondari ya penae pamoja na kukagua moja timu shiriki za mashindano hayo na mwisho kupiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya Copa UMISSETA.
Wananchi  wengi walijitokeza kufuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *