habari

Shirika La WHO Labainisha, Asilimia 90 Ya Watu Duniani Wanavuta Hewa Chafu.

on

Ripoti iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO imesema asilimia 90 ya watu duniani wanavuta kiasi kikubwa cha hewa chafu. WHO imeonya kwamba sumu zinazopatikana kwenye hewa zinaweza kusababisha maradhi ya kiharusi, moyo na saratani ya mapafu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu milioni 7 hupoteza maisha kila mwaka duniani, na 9 kati ya 10 huvuta hewa chafu zaidi. Mkuu wa shirika hilo Tedrom Adhanom Gebreyesus amesema kwenye taarifa hiyo kwamba kitisho cha hewa kipo kwa kila mmoja lakini mataifa masikini na maeneo yenye idadi kubwa ya watu ndio hubeba mzigo mkubwa zaidi.

Zaidi ya asilimia 90 ya vifo vitokanavyo na hewa chafu hutokea kwenye mataifa yenye kipato duni na cha kati hususani yaliyoko Asia na Afrika kufuatia uchunguzi uliofanyika katika nchi 108.

Na DW.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *