We have 173 guests and no members online

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Kivuko cha mv Misungwi, wakati akitoka Mwanza kwenda Sengerema mkoani humo, kuendelea na kampeni leo

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi (Hawapo Pichani) aliosafiri nao katika Kivuko cha Misungwi, wakati akienda Sengerema kutoka jijini Mwanza, kwenda Sengerema kuendelea na kampeni zake leo

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan (wapili kushoto), akiwa katika Kivuko cha mv Misungwi, wakati akitoka jijini Mwanza kwenda sengerema kuendelea na kampeni zake leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Kampanei za CCM Kitaifa, Christopher Ole sendeka na watatu pia i Mjumbe wa kamati hiyo, Angela Kizigha na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Baraka Konisaga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza.(P.T)

Posted On Sunday, 11 October 2015 04:28

Posted On Sunday, 11 October 2015 04:20

Posted On Saturday, 10 October 2015 17:30

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Viwanja vya Nyabogoya, eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.

 Wananchi wakimshangilia Mama Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia maelfu ya wananchi hao waliofurika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Viwanja vya Nyabogoya, eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.

 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Kitaifa, Christopher Ole Sendeka, katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika Viwanja vya Nyabogoya, eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Maarufu wa jina la Msukuma, akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia Suluhu Hassan leo katika Viwanja vya Nyabogoya, eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.

 Kada wa CCM, Paul Makonda akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika Viwanja vya Nyabogoya, eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.(P.T)

Posted On Saturday, 10 October 2015 02:18

Sehemu ya wananchi wa Mji wa Karatu, wakionyesha furaha yao baada ya kuiona Chopa inayotumiwa na Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.

Kikundi cha Ngoma ya Asili kikitoa Burudani katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akivishwa vazi rasmi la kimila la kabila la wa Iraki, wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani Manyara leo Oktoba 9, 2015.(P.T)

Posted On Saturday, 10 October 2015 01:46

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango wakiwasalimu wakazi wa Same waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Ndungu.PICHA NA MICHUZI JR-KILIMANJARO.

  Wakazi wa Same Mashariki wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimvalisha fulana mmoja wa wafuasi wa CHADEMA alieamua kurejea chama cha CCM jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya jimbo la Same Mashariki

  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ndungu kweye mkutano wa kampeni Same Mashariki,jioni ya leo.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo,Innocent Shirima wakiwapungia wananchi walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa kampeni mjini himo.(P.T)

Posted On Friday, 09 October 2015 03:17

Kamishna wa NCCR-Mageuzi wa Mkoa wa Ruvuma, Mchatta Eric Mchatta (kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, Leticia Ghatti Mosore, na mwakilishi wa NCCR-Mageuzi, Hamlyn Erasto.

Leticia Mosore (katikati) akisoma taarifa yake.

Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo. (P.T)

Posted On Friday, 09 October 2015 03:11
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Godbress Lema, wakiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 8, 2015.


Edward Ngoyai Lowassa na Godbless Lema wakiwasili katika viwanja vya Sinoni Unga Ltd leo Alhamisi 8/10/2015(P.T)

Posted On Friday, 09 October 2015 03:06

Wasanii wa Kikundi cha Big Star wakitowa burudani kwa wimbo maalum wa Kapeni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.zilizofanyika katika viwanja vya mpira vya Urafiki mikunguni Unguja

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya mkutano wa mkgombea Urais wa Zanzibar kwa kupitia CCM wakishangilia kwa kupeperusha bendera za Chama wakati wa mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya mpira urafiki mikunguni Zanzibar,

Mwanachama wa CCM akishangilia kwa kuonesha picha ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe Borafya Silima akiwahutubia wananchi katika viwanja vya urafiki mikunguni akielezea mafanikio ya CCM yaliopatika kutokana Ilani ya Uchaguzi ya miaka mitano ya Dk Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja hivyo. 

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Seif Aki Iddi wakiwa katika jukwaa kuu wakati wa mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Jimbo la Shaurimoyo Wilaya ya Mjini Amani Kichama katika viwanja vya mpira vya urafiki mikunguni. (P.T)

Posted On Thursday, 08 October 2015 08:55

Wasimamizi wa Uchguzi nchini wametakiwa kusimamia sheria katika kutekeleza majukumu ya kusimamia Uchaguzi unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Mwenyekiti wa Uchaguzi Jaji mstaafu Damiani Lubuva amesema hayo katika hotuba ya ufunguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi toka majimbo yote nchini kwa lengo la kupata uzoefu kuboresha utendaji kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Mpaka sasa zoezi la kampeni linakwenda vizuri tufanye kazi zetu kwa weledi, kila mmoja wetu ashiriki kikamilifu katika mkutano huu, ili kuweza kupata michango itakayoweza kufanikisha uchaguzi huru, haki na amani ukizingatia kwamba wengi wenu ni wazoefu, kupitia wakati huu mtaweza kushirikishana uzoefu na kujifunza”

Aidha Lubuva ameongeza kuwa NEC imehusisha jeshi la polisi kwa lengo la kupata maoni yao ya namna ya kusimamia Uchguzi na kuwataka washiriki wote kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha amani inakuwako na itaendelaa kuwako hata baada ya `uchaguzi.

Wakurugenzi hao wametakiwa kutomruhusu mtu au kikundi cha watu, vijana kusimama karibu na vituo vya kupigia kura kwa madai ya kulinda kura hii ni kukiuka taratibu na sheria na kuwasihi wawe na ushirikiano na kuwa karibu na NEC wakati wote wa shughuli za Uchaguzi kwa lengo la kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani nchini.Posted On Thursday, 08 October 2015 08:27

Ndege ya Urusi

Urusi imesema ndege zake zinashambulia ngome za wapiganaji wa Islamic State

Mawaziri wa ulinzi wa mataifa wanachama wa muungano wa kujihami wa Nato wanakutana leo kujadili mashambulio yanayotekelezwa na Urusi nchini Syria.

Mkutano huo utakaofanyika mjini Brussels unafanyika baada ya mmoja wa wanachama wa Nato Uturuki kusema ndege za kijeshi za Urusi ziliingia anga yake.

Urusi imefyatua mizinga kutoka manowari yake pamoja na kutekeleza mashambulizi kutoka angani kumsaidia kiongozi wa Syria Bashar al-Assad.

Lakini Moscow imekanusha matai ya nchi za Magharibi kwamba mashambulio hayo yanawalenga wapinzani wa Assad, baadhi wanaosaidiwa na mataifa ya Magharibi, na wala si wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).

Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya ulinzi Jonathan Marcus amesema Nato inadhamiria kueleza wazi kwamba itajibu mashambulio yoyote.

Alhamisi, Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisema muungano huo ulieleza kutofurahishwa kwake na kuongezeka kwa “uwepo wa kijeshi” wa Urusi nchini Syria.BBC

Posted On Thursday, 08 October 2015 08:22

Baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan Kata ya Igagala, Uvinza Mkoani Kigoma wakimtaka awasalimie kabla ya kuendelea na safari. Mgombea mwenza huyo wa CCM ameingia mkoani Kigoma kwa ziara ya kampeni kuinadi ilani ya CCM.

Baadhi ya Wananchi wakiwa wamesimama pemezoni mwa barabara kumlaki mgombea mwenza wa urais CCM alipokuwa akiwasili Mkoani Kigoma kufanya mikutano yake ya kampeni.

Mgombea mwenza akizungumza na wananchi waliomsimamisha njiani kuwasilisha kero zao.

Mgombea mwenza CCM, Mama Suluhu akiwa ameshikilia kadi na bendera za vyama vya upinzani alizokabidhiwa na vijana waliohama vyama vyao na kujiunga na CCM, alipokuwa akiwasili Mkoani Kigoma mwisho wa reli.(P.T)

Posted On Wednesday, 07 October 2015 05:00
Page 8 of 116

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu