We have 176 guests and no members online

Msoma Utenzi akisoma Utenzi maalum wakati wa Uzinduzi wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja uliofanyika katika Viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Zanzibar.

Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akiwa katika viwanja vya mkutano akishangilia na Picha ya Mgombea wake wa Ubunge kupitia CCM Ndg. Ussi Salum Pondeza AMJADI wakati wa mkutano huo

Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakiwa katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Unguja.(P.T)

Posted On Monday, 05 October 2015 05:15


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Peoples, mjini Singida, ambapo alilisitiza kwamba akishinda urais ataongeza ajira kwa vijana kwa kuwapa mikopo ya mitaji ya kuanzishia miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi.


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwahesabia kupiga Push Up wagombea ubunge Mwiguru Nchemba wa Iramba (kulia), Musa Sima (katikati) wa Singida Mjini na Lazaro Nyalandu wa Jimbo la Singida Kaskazini wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Peoples mjini SingidaDk Magufuli akikagua daraja la Msingi katika Kijiji cha Msingi wilayani Mkarama, Singida

Mkazi wa Kata ya Sepuka Singida Magaribi akiwa na mwanawe katika mkutano wa Dk MagufuliWananchi wakishangilia kwa furaha baada ya kumuona Dk Magufuli akatika Kata ya Ndago, wilayani Iramba(P.T)

Posted On Sunday, 04 October 2015 04:28

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mumungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Mh. Edward Ngoyayi Lowassa amewataka wananchi kisiwani Pemba kumkataa na kutomchagua mgombea yeyote anayechezea amani ya nchi kwani nchi hii si miliki ya mtu bali ni mali ya watanzania wote, na kusisitiza kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anapambana na umasikini kwa nyanja zote.

Mh.Lowassa aliyewasili kisiwani Pemba na kusindikizwa na vijana kwa pikipiki za Vespa na magari hadi hapa kiwanja cha Kibirinzi ambapo mkutano wa kampeni ulifanyika, aliwataka wananchi wa Pemba kumkataa mgombea anayetishia amani na utulivu, kwani ndiyo itakayoweza kusaidia kufikisha malengo ya kuleta mageuzi ya kweli katika nyanja zote za maendeleo, na kuahidi kuwa ataimarisha hospitali kila wilaya kwa kuweka vifaa vya kisasa.

Mh. Lowassa amesisitiza kuwa endapo atakuwa rais wa Tanzania, atahakikisha anabadilisha mitaala ya elimu kuwa ya kisasa ili kuliletea maendeleo ya haraka taifa la Tanzania.

Awali, mgombea mwenza Mh. Juma Duni Haji aliwataka Wazanzibari kushirikiana ili kufanya mabadiliko kwa amani na utulivu. Naye mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi, CUF Malim Seif Sharif Hamad ameendelea kusisitiza kuwa chama chake hakina mpango wa kufanya vurugu kama inavyodaiwa.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi, wakati akiwa njiani kuelekea kwenye Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo Oktoba 3, 2015..

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akifurahi jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, walipokutana katika katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo Oktoba 3, 2015. .(P.T)

Posted On Sunday, 04 October 2015 04:17

 Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambako alika kusalimia familia hiyo na kuzuru kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, leo, katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama, akiwa kaika ziara ya kufanya mikutano ya kampeni katika mkoa wa Mara.

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia mtoto wa sita wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere, alipowasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa huyo, katika Kijiji cha Mwitongo, Bitiama mkoani Mara.

 Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere

 Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.(P.T)

Posted On Saturday, 03 October 2015 03:58

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni.
PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru kiongozi huyo wa dini kwa kujitolea kumuombea Dua ya heri na afya njema katika nafasi yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida jioni ya jana ,wakati akiwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani. 

Dkt. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali  hasa za mashirika ya  dini ambazo zinaendesha hospitali  katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili   kuimarisha huduma  za kiafya  kwa jamii.

Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya jana,ambapo leo anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV.(P.T)

Posted On Saturday, 03 October 2015 03:37

Pichani Ndugu  Saidi Mwamende akimuliza swali   Mhe: Jussa,  (Hayupo Pichani)

Na Swahilivilla. Blog Washington Waziri Majivuno wa Kusadikika alisema: "Hekima ni kitu adimu kupatikana kwa mtu asiye na mvi...". Pia Waswahili wanasema: "Akili ni nywele"
Mshitakiwa Karama aliipinga hoja ya Waziri Majivuno kwa kusema: "....Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima..."
Nimekuwa nikiyatafakari mafungu hayo matatu ya maneno ili kuona kama yana uhalisia wowote katika maisha yetu ya leo.

Hivi majuzi swahibu yangu Said Mwamende alinipigia simu na mara tu baada ya kuijbu, nilihisi sauti yake imejaa furaha, ndipo nikamwuliza ''umepandishwa cheo?" Akanijibu: "Hapana, bali nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania zinavyokwenda na nikakumbuka ule mkutano wa Mheshimiwa Ismail Jussa alioufanya na Wanadiaspora hapa Washington.

Yale aliyoyasema ndiyo yanayoendelea kutokea hivi sasa". Nikakurupuka kuchakura maktaba yangu kuitafuta rekodi ya mkutano ule ili nijikumbushe aliyoyasema Mheshimiwa Jussa. Baada ya kuiangalia tena, nikaona sehemu ambayo Swahibu yangu Said Mwamende alimwuliza Mheshimiwa Jussa swali ambalo lilihitaji mwono na mtazamo wa kina wa kisiasa: "Je, UKAWA, tuseme, kwa upande wa chama chako wewe atakuwepo Mheshimiwa Lipumba, na tuseme kwa upande wa CHADEMA Mzee wetu Mbowe. Watu hawa tayari wameshagombea Urais.

Je hamuoni kwa CCM kwa sasa hivi kuna hombwe la aina fulani? Kuna Mheshimiwa Lowassa inawezekana kwamba hatogombea CCM kutokana na labda hawatomtaka. Mnafikiriaje UKAWA kama mtamchukua yule Lowassa ili mumuweke pale agombee?" Kwa ulimi wa fasaha kuliko wa Karama wa Kusadikika, Mheshimiwa Jussa alilijibu swali la Bwana Mwamende ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania katika Jiji la Washington na Vitongoji vyake (DMV), kwa kusema: "Katika siasa, wiki moja inaweza kuwa muda mrefu sana".

Aliendelea kwa kusema kuwa siyo Lowassa tu, anaweza kupitishwa Loawassa akaachwa mtu mwengine mwenye ugomvi na Lowassa vilele. Kwa sababu CCM hivi sasa siyo chama tena kinachowaunganishwa na itikadi. Kinachowaunganisha ni Escrow na kwamba kila mmoja atapata mgao wake kiasi gani".

 Mhe: Ismail Jussa  akijibu swali la  Saidi Mwamende  (Hayupo pichani)

Katika mkutano huo uliofanyika tarehe 28 Februari mwaka huu jijjini Washington, Bwana Ismail Jussa, aliwathibitishia Wanadiaspora wa Tanzania nchini Marekani pamoja na ulimwengu kwa ujumla kuwa Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima, lakini nadharia hiyo wakati wake umepita na hautorejea tena.(P.T)

Posted On Saturday, 03 October 2015 03:32

Waangalizi kutoka Jumuiya ya Ulaya EU wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Chadema uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga leo majira ya saa tano asubuhi, mgombea huyo anaungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD. (Picha na Francis Dande)

 Tambwe Hiza akihutubia katika mkutano huo.

 Mgombea ubunge jimbo la Temeke, Abdalah Mtolea.

 Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam.(P.T)

Posted On Friday, 02 October 2015 05:28

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia baadhi ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda.

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia baadhi ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda.

Sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano wa mgombea mwenza wa CCM, Jimbo la Mwibara leo.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mwibara, Alphaxard Kangi Lugola akiwahutubia wanaCCM na wananchi wapenzi wa chama hicho waliokuwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu leo Jimbo la Mwibara. 

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi na wanaCCM Mji wa Mugumu, Wilaya ya Serengeti leo. Ambapo katika hotuba yake amewahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa muda mfupi baada ya kuingia madarakani atatoa maelekezo kwa waziri wa kazi kuhakikisha makampuni yaliyowekeza Serengeti yanatoa ajira bila upendeleo huku wakizingatia kutoa kipaumbele kwa wanaSerengeti.(P.T)

Posted On Friday, 02 October 2015 05:14

Viongozi wa vyama vya siasa vitano AFP, UMD, CHAHUSTA, JAHAZI ASILIA NA DEMOKRASIA MAKINI kwa pamoja tumeungana kutoa wito kwa wanasiasa wenzetu, viongozi wa dini na wananchi wote kwa jumla kuhusiana na uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika ifikapo tarehe 25/10/2015

Tamko hili ni pamoja na:-

1. Tubnawapongeza wagombea wote wa nafasi ya Urais kwa kuendelea kufanya kampeni kwa njia ya amani na Utulivu.

2. Tunawataka watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 25/10/2015 kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani na Utulivu.

3. Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali, Urais, Ubunge na Madiwani waache kutoa maneno ya kuwatia hofu wapiga kura kwamba tunaweza kuibiwa kura na badala yake tuwahamasishe zaidi kujitokeza kwa wingii kupiga kura na kuiamini tume ya taifa ya uchaguzi kuwa watatenda haki kwa wagombea wote bila kujali hadhi ya chama cha siasa anachotoka mgombea.

4.Viongozi wa dini wanaotaka kuwafanyia kampeni wagombea wasifanye hivyo katika nyumba za ibaada na badala yake wakipenda kufany ahivo watumie majukwaa ya kisia sa na sio madhabahu.

5.Viongozi wa vyama vya siasa waache kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa kuwatia hofu ya kutabiri kuwepo kwa umwagikaji wa damu.

6. Viongo wa asasi za kiraia wasiendelee kufanya tafiti na kuwapa ailimia wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili na kanuni za kitafiti mabyo matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku katika jamii kwa kueta za ama kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa katika tafiti husika.

7. Mwisho tunawataka watanzania wote kuwa makini na kuyadharau matamko yote yenye nia ya kuwatia hofu na kuendelea kuipenda nchi yetu ya Aamini na Utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Taifa letu. Na vilevile viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa letu libaki kuwa na utulivu wakati wote wa uwepo wetu katika nchi yetu.(P.T)

Posted On Friday, 02 October 2015 05:08

Baadhi ya wanachama wa CCM wakishangilia katika uzinduzi wa kampeni za Chama hicho zilizofanyika katika uwanja wa Polisi Himo.(P.T)

Posted On Thursday, 01 October 2015 07:08

>

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwasenge, Jimbo la Musoma Mjini. Katika hotuba yake aliwaomba wanaMusoma kuichagua CCM ili iweze kuunda Serikali kwani imepanga kuboresha huduma mbalimbali za kijamii pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo hilo itakayochangia kukua kwa biashara anuai.

Alisema Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kujenga maeneo ya kisasa ya maegesho ya meli (magati) Musoma na ndani ya miezi mitatu huduma ya maji maeneo mbalimbali itapatikana kwa uhakika kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji eneo hilo. Aliongeza pia ili kuboresha huduma za Mwisenge zahanati ya eneo hilo itabadilishwa mara moja na kuwa kituo cha afya.(P.T)

Posted On Thursday, 01 October 2015 07:01
Page 9 of 116

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu