We have 177 guests and no members online

Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo jana Septemba 28, 2015.

Umati wa Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwani, jana Septemba 28, 2015.(P.T)

Posted On Tuesday, 29 September 2015 04:13

Ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati msafara wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli ukitoka kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa baada ya mkutano wa kampeni kumalizika

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ( wa pili kulia) akiwaongoza wasanii kupiga Push Up  wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Samora, mjini Iringa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wasanii wanaomfanyia kampeni nchini kwa kutumia usafiri wa kibabaji  wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Samora, mjini Iringa(P.T)

Posted On Tuesday, 29 September 2015 04:06

Posted On Tuesday, 29 September 2015 04:05

mafinga iringa (2)

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli, akiwahutubia wananchi wa Iringa, leo. 

Magufuli akisalimiana na John Maleccela

Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu, John Malechela.

magufuli akizungumza na wakazi wa kijiji cha lujewa jimbo la mbalali

Magufuli akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Lujewa jimbo la Mbalali

mwanjelwa mbeya

Wananchi wa Mwanjelwa mkoani Mbeya wakimsikiliza Magufuli.(P.T)

Posted On Monday, 28 September 2015 03:27

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Mhe Shamsi Vuai Nahodha akisalimiana naViongozi wa CCM wa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuwasili katika viwanja vya mkutano wa hadhara wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika viwanja vya mpira bungi. 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika viwanja vya mpira bungu kuhudhuria Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

Wanachama wa CCM wakiingia katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakiwa na picha za Wagombea 

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla alipowasili katika viwanja vya Bungu kuendelea na Kampeni zake za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.(P.T)

Posted On Sunday, 27 September 2015 12:46

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati alipowasili eneo la Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.

Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.(P.T)

Posted On Sunday, 27 September 2015 03:48

Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukiwa umezuliwa njiani na wananchi katika eneo la Rudewa, wakati akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Mikumi mkoani Morogoro jana, Septemba 25, 2015. (Picha na Bashir Nkoromo).

Mkazi wa Kilosa mkoani Morogoro, akiwa amembeba mtoto wake mabegani huku akimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya wananchi kuzuia msafara wake katika eneo la Rudewa, akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Mikumi mkoani Morogoro jana, Septemba 25, 2015. (Picha na Bashir Nkoromo).

Mwananchi akiwa amemkinga jua mtoto aliyembeba mgomgoni wakati akimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipozungumza na wananchi waliozuia msafara wake katika eneo la Masanze mkoani Morogoro, jana, Septemba 25, 2015. (Picha na Bashir Nkoromo).(P.T)

Posted On Saturday, 26 September 2015 06:10

Posted On Saturday, 26 September 2015 03:48

magufuli akifanya mkutano wake wa mwisho mjini kahama leo katika viwanja vya UWT CCM Kahama

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Jonh Pombe Magufuli akifanya mkutano wa kampeni katika viwanja vya UWT CCM, Kahama.

Mjumbe wa kamati kuu ya ccm na mwenyekiti wa jumuiya ya wazaz ccm, Abdalah Bulembo akiwataka wananchi kuichagua ccm Ktika uchaguz mkuu ujao

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdalah Bulembo akiwataka wananchi kumchagua Magufuli.

Samuel sitta akiwaomba wananch waliokusanyika viwanja vya UWT CCM Kahama kumchagua magufuli

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msitaafu, Samuel Sitta akimnadi Magufuli.

katibu mwenez wa chadema Musa Dida akirudisha kadi nya chadema ccm na kuvua gwanda

Katibu Mwenezi wa Chadema, Musa Dida akirudisha kadi ya chama chake, kuvua gwanda na kuchukua kadi ya CCM.(P.T)

Posted On Saturday, 26 September 2015 03:44

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mererani, katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 25, 2015.

Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara wakionyesha furaha yao mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mererani, leo Septemba 25, 2015.(P.T)

Posted On Friday, 25 September 2015 20:01

Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.

Mwenendo wa Kampeni

Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni. Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi. Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.

Tunaridhika sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu na mikakati mipya.

Midahalo ya Wagombea

Tumeshangazwa na kauli ya Ndugu Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania kwamba CCM haijathibitisha kushiriki mdahalo. CCM ilipokea mwaliko wa MCT na kuijibu kwa barua ya tarehe 13 Septemba 2015 yenye kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 iliyosainiwa na Ndugu Stephen Msami, Msaidizi wa Katibu Mkuu. Barua hiyo ilipelekwa na kupokelewa kwa dispatch ambayo nakala yake tunayo. Baada ya hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wawakilishi wa MCT katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba ili kutaka kujua zaidi na kutoa maoni ya CCM kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo. Katika kikao hicho, ambapo MCT iliwakilishwa na Afisa wake, Ndugu Allan Lawa, pamoja na Ndugu Tido Mhando, CCM ilithibitisha tena kushiriki mdahalo. Tatu, tarehe 16 Septemba 2015, CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa, ikithibitisha kushiriki mdahalo. Kauli ya Ndugu Mukajanga inalenga kuwasaidia kisiasa wale ambao hawajathibitisha au hawana nia ya kuthibitisha kushiriki. Kwa msingi huu, tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa taasisi mbalimbali zilizokuwa na nia ya kuandaa midahalo, (kama vile CEO Roundtable, UDASA, Twaweza) ili kuiondolea uwezo taasisi moja, au kikundi cha watu wachache, kuhodhi na kuwa na ukiritimba kwenye jambo hili kubwa na muhimu.

CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:

1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais
2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.
3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki.

Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa.

Utafiti wa TWAWEZA

CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:

1. Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua.

2. Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.

3. Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa.

4. Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.

5. Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.

Lakini vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi.

Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi.

Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu. CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini.

Utafiti ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki.

Itakumbukwa kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa asilimia 61. Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa na Synovate.

Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.

Imetolewa na:

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
23.09.2015(P.T)

Posted On Friday, 25 September 2015 07:54

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kutoshangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotoa ushindi wa asilimia 65 kwa Mgombea Urais wao, Dk John Magufuli, huku kikiahidi kuongeza kasi, nguvu na mikakati zaidi katika nusu ya pili ya kampeni.

Hata hivyo, kimeshangazwa na taharuki hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huo na kusema kilitegemea wasomi na wanaharakati hao wangefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa ulioanza kujitokeza nchini kwa vile unajenga.

Pia kimesisitiza kuwa kimethibitisha kushiriki mdahalo wa wagombea urais ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), lakini kikisitiza uwashirikishe wagombea wenyewe na si wawakilishi wao, na pia wagombea wote, hasa wa vyama vikuu wawepo na washiriki.(VICTOR)

Posted On Thursday, 24 September 2015 09:10
Page 10 of 116

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu