We have 212 guests and no members online


..na kabegi kamoja tu. Ni John Mjengwa. Ametokea Paris kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi. Alipokuwa Paris amekuwa akitutumia habari kuhusiana na mkutano huo. Kwa sasa yuko nchini kwa likizo ya shule.
Karibu nyumbani John!
Maggid

Posted On Tuesday, 15 December 2015 05:04

 

Posted On Monday, 14 December 2015 03:05

Posted On Sunday, 13 December 2015 03:40

WANANCHI katika majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini, watafanya uchaguzi wa wabunge wao kesho. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana.

Pia alisema wananchi wa Kata ya Mvomero mkoani Morogoro, nao watamchagua diwani. Wananchi wa maeneo hayo, hawakupiga kura katika uchaguzi mkuu, uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Siku hiyo, uchaguzi uliahirishwa katika majimbo saba, ikiwemo Arusha Mjini na Handeni Mjini, kata ya Mvomero na nyinginezo 34 nchini. Tangu wakati huo, uchaguzi umeshafanyika katika baadhi ya majimbo na kata.

Lubuva aliwaomba wananchi waliojiandikisha kama wapigakura katika majimbo na kata husika, kujitokeza kesho kwenye vituo walikojiandikisha ili kuweza kupiga kura na kuwachagua na viongozi wanaowataka.

IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

Posted On Saturday, 12 December 2015 08:03

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya Rais John Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa Arusha, Philemon Mollel (Monaban), uliofanyika katika kata ya Daraja Mbili jana, Kinana alisema sera ya kupambana na ufisadi ilizungumzwa katika kampeni na Dk Magufuli peke yake na si Lowassa wala kiongozi yeyote wa Ukawa.

Kinana alisema anamshangaa kiongozi huyo kwa kuwa mbali na kushindwa kuzungumza wakati wa kampeni za urais, pia hakuwa na hotuba yoyote ambayo ingeweza kukaririwa na Dk Magufuli.

Alisema Lowassa hakuweza kuzungumzia masuala yoyote ya kupambana na ufisadi kwa kuwa yeye ni mtuhumiwa na vyama vina vyounda umoja huo ndiyo vimekumbatia ufisadi kwa sasa.

Kwa mujibu wa Kinana, Lowassa alinadi sana mabadiliko kama angeweza kuingia madarakani, lakini hakufafanua ni mabadiliko yapi ambayo angeweza kuyaleta, wakati anatoka katika mfumo ule ule aliokulia kwa zaidi ya miaka 40 akiwa ndani ya CCM na Serikali yake.

“Jamani Lowassa alisema mabadiliko lakini hao wanaotaka mabadiliko wana umri wa ujana sawa na jua linalochomoza la saa mbili asubuhi, wakati yeye anayedai kuleta mabadiliko ana umri wa uzee sawa na jua linalozama la saa 12.30 jioni, si vichekesho hivyo?” Alihoji Kinana.

Alisema kutokana na ukweli huo, ndiyo maana Watanzania walipima na kuamua kumpa ushindi wa kishindo Dk Magufuli, kutokana na uadilifu wake pamoja na uwezo wake wa kuchapa kazi na kuamua kumnyima Lowassa na ndiyo maana kwa sasa anajifariji kwa kusema sera zinazotekelezwa ni za Ukawa.

Akizungumzia kazi alizoanza kuzifanya Rais Magufuli, Kinana alisema zimewakuna Watanzania wengi na kusema kuwa hiyo ndiyo kazi aliyoahidi kwao kuifanya na kwamba anaamini ataifanya kwa dhati katika kuwapigania wananchi wanyonge.

Mfumo CCM Akizungumzia madai kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayetokana na CCM anayeweza kupambana na machafu ndani ya Serikali, kwa kuwa hilo ni suala la mfumo, Kinana alipinga na kusema si kweli.(VICTOR)

Posted On Saturday, 12 December 2015 08:01

 

 

 

 

Posted On Saturday, 12 December 2015 03:36

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe A bass Ali Hassan Mwinyi, akitembelea Kituo cha Afya cha Fuoni Zanzibar kinachotowa huduma kwa Wananchi wa Jimbo hilo na jirani wakati akitimiza ahadi yake kwa kutuo hicha, akipata maelezo kutokwa kwa mdhamini wa kituo hicho Muuguzi wa Afya ya Jamii Bi Mwaka Pandu Makame akitowa maelezo ya eneo lao la kuchomea taka za kituo hicho.

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassan Mwinyi akitembelea kituo hicho cha Afya Fuoni Zanzibar akiwa katika ziara yake katika jimbo lake kujiuonea ufanisi wa kituo hicho na kukabidha Madawa na kuvifanyia mategenezo vyoo vya kituo hicho ni moja ya kero za Wananchi wanaofika kituoni hapo.(VICTOR)

Posted On Friday, 04 December 2015 09:58

Na Maelezo Zanzibar 30/11/2015

Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano.

Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla.

Amesema toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo.

“Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai.

Amesema kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa upya.

Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria.

“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai.

Katika taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema kuwaChama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri.

Vuai amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR(P.T)

Posted On Monday, 30 November 2015 15:28

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi ameimbia RFI Kiswahili kuwa, viongozi wa kisiasa kutoka serikali na upinzani wamekubaliana uchaguzi Mkuu kurudiwa tena.

Hata hivyo, Makamu huyo wa pili amedokeza kuwa hadi sasa haijaafikiwa ikiwa tume ya sasa ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Jecha Salim aliyefuta matokeo hayo itakubaliwa kusimamia uchaguzi mpya.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameeeleza kuwa rais Ali Mohamed Shein anaendelea kuwa uongozini kikatiba.Wananchi wa Zanzibar wanasubiri uamuzi wa viongozi wa kisiasa kuhusu mvutano huu wa kisiasa katka visiwa hivyo.

IMECHOTWA NA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

Posted On Friday, 27 November 2015 14:09

Mauricio Macri katika mji wa Buenos Aires Novemba 22, 2015.

Mauricio Macri katika mji wa Buenos Aires Novemba 22, 2015

Na RFI

Mauricio Macri kutoka chama cha Kiliberali amechaguliwa Jumapili hii kuwa rais wa Argentina katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais. uchaguzi ambao umeashiria mwisho wa utawala wa Kirchner alieliongoza taifa hilo la tatu kwa uchumi katika eneo la Amerika ya Kusini.

Tafiti angalau nne wa ziliofanywa na televisheni baada ya uchaguzi, zinampa ushindi Meya wa Buenos Aires. Matokeo ya kwanza rasmi yalikua yanatarajiwa kutangazwa saa 1:30 usiku saa za Argentina (sawa na 4:30 usiku saa za kimataifa).

Mauricio Macri, mwenye umri wa miaka 56, amemshinda Daniel Scioli, mgombea wa serikali ya mseto, ambaye alikuwa alipewa nafasi kubwa ya kushinda kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi.

Daniel Scioli akipiga kura katika kata ya Tigre, katika jimbo la Buenos Aires Novemba 22, 2015.

Rais Cristina Fernández de Kirchner kutoka chama cha mrengo wa kushoto, anaiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2007 baada ya kumrudilia mume wake, ambaye hakuweza kugombea awamu ya tatu mfululizo, kwa mujibu wa katiba.

Mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza, wafuasi wa meya wa Buenos Aires, walikutana katika makao makuu ya muungano wa vyama vya upinzani wa Cambiemos (ikimaanisha tubadili) unaongozwa na Macri, wamejipongeza na kuanza kusherehekea ushindi.

Wafuasi wa Mauricio Macri jijini Buenos Aires, Novemba 22, 2015.

Mauricio Macri atajitahidi kushirikiana na taasisi zingine za uongozi wa nchi kwa kuliongoza taifa hilo, kwani muungano wake hauna wingi wa viti katika Baraza la wawakili na Baraza la Seneti.(P.T)

Posted On Monday, 23 November 2015 04:43

Posted On Monday, 16 November 2015 04:24

Museveni

Juhudi za Mbabazi na Besigye kutaka kuafikiana mmoja wao ashindane na Museveni zimegonga mwambaRais wa Uganda Yoweri Museveni amesema wagombea urais wanaoshindana naye kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao si tishio kwake.

“Hiki hakitakuwa kinyang’anyiro kikali,” ameambia kikao cha wanahabari mjini Kampala.

Wapinzani wakuu wa Bw Museveni wanatarajiwa kuwa Amama Mbabazi na Kizza Besigye, ambao walikuwa marafiki wake wakuu wak

ati mmoja.

"Nasikia watu wakizungumza kuhusu kupiga vita ufisadi. Utawezaje kukabiliana na ufisadi ilhali twasikia ukiomba huyu na yule wajiunge nawe?” amesema.

"Lazima uwe na uwezo,” ameongeza Bw Museveni.

Hii ni mara ya kwanza kwa Bw Mbabazi, aliyekuwa waziri mkuu wakati mmoja, kuwania urais.

Bw Museveni ameongoza Uganda tangu 1986

Museveni

Museveni aliwasilisha karatasi za uteuzi kwa tume ya uchaguzi janaTume ya uchaguzi ya Uganda imeidhinisha watu wanane kuwania urais mwaka ujao wakiwemo Bw Museveni, Bw Besigye, Bw Mbabazi na Venansius Baryamureba.

Kampeni zitaanza Novemba. BBC

Posted On Thursday, 05 November 2015 05:15
Page 2 of 114

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi