We have 153 guests and no members online

a1 03b24

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanachama wa UVCCM wa vyuo vikuu mkoani Tabora waliomtembelea Ikulu ndogo mkoani humo usiku wa kuamkia leo. Pamoja na mambo mengine Rais Kikwete aliwataka vijana hao kuzingatia masomo kwa nguvu zao zote, akisisitiza kwamba elimu ni ufunguo wa maisha hivyo wasome kwa bidii ili nchi ipate wasomi waliobobea katika kila nyanja katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo

Posted On Thursday, 10 January 2013 02:27

IMG-20130109-00249 9c868

                                                                                    IMG-20130109-00246 f474c

Posted On Wednesday, 09 January 2013 14:42

Wana nchi wa kata ya Itenka A jimbo la katavi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mh waziri mkuu Mizengo Pinda alipo kuwa ana hutubia kuhimiza watu kulima kwa kutumia kilimo cha kisasa mwishoni mwa wiki wana nchi wengine walilazimika kupanda juu ya miti (Picha na Chris Mfinanga)

Posted On Wednesday, 09 January 2013 13:18

nz1 b04f8

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelzo ya ujenzi wa barabara ya Tabora-Ndono kabla hajazindua rasmi i ujenzi wa  barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.

nz2 c6a58

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikat utepe kuzindua rasmi  ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji

Posted On Tuesday, 08 January 2013 19:15

Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Constantine Makitanda akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya  Chama hicho kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (Jumanne Januari 8, 2013).

 

Posted On Tuesday, 08 January 2013 13:47

Hon-KIGODA-1024x768 5f92b

                                  Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Abdallah  Kagoda

Na : Gladness Mushi,Arusha.

Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Abdallah  Kagoda amesema kuwa mipaka  ya nchi imekuwa chanzo cha uingizwaji wa bidhaa ambazo ziko chini ya viwango (feki)  hali inayochangia kuleta athari kubwa kiuchumi na afya za watu wanaotumia bidhaa hizo.

Posted On Tuesday, 08 January 2013 11:57

mg1 9f504

 

 Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza  mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola  jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri  ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha.

Posted On Tuesday, 08 January 2013 10:57

seif bfc64

CHAMA cha Aliance For Democratic (ADC) kimemwonya Katibu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kwamba iwapo ataendelea kukishambulia majukwaani, kitaanika maovu yake yote aliyoyafanya ndani ya chama chake na Watanzania kwa ujumla.

Posted On Tuesday, 08 January 2013 08:36

makala 1f08f

KAMANDA mpambanaji wa Chadema kutokea Babati Jackson Wilson Makala (pichani juu), amekanusha vikali habari zilizosambaa kwa watu tofauti waliokaribu nae zikimhusisha na sekeseke la kuwavua uanachama wa Baraza la Vijana Chadema ambalo limeleta sintofahamu dhidi yake baada ya  gazeti moja la kila siku kumuandika jana kuwa nae ni miongoni mwa vijana waliosimamishwa kwa muda katika baraza hilo (BAVICHA kwa makosa tofauti ya utovu wa nidhamu.

Posted On Tuesday, 08 January 2013 08:22

ajk1 d4b96

 Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Posted On Monday, 07 January 2013 11:14

kinana 948a8

KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana amekerwa na chokochoko za kidini zilizoanza kujipenyeza hivi karibuhi na kutoa wito kwa madhehebu ya dini na taasisi zake hapa nchini,kuendelea kuhubiri amani kwa kuliombea taifa , ili wananchi waendelee kujivunia amani iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Kinana alitoa kauli hiyo juzi kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Imam Husein, yanayoadhimishwa na dhehebu la KhojaShia Ithna Asheri Jamaat Arusha kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jumuiya hiyo jijini hapa , ambapo watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa madhehemu pamoja na viongozi wa chama na Serikali walihudhuria.

Kinana alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa viongozi wa dini na taasisi zake kuendelea kuienzi amani kwa kuhubiri suala la kudumisha amani na kuonya kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua za haraka kwa mtu ama kikundi chochote cha dini kitakachojihusisha na uvunjivu wa amani.

Posted On Saturday, 05 January 2013 10:09

Bernard-Membe14 d0bb1

WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.

Posted On Saturday, 05 January 2013 09:36

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu