We have 81 guests and no members online

Posted On Tuesday, 03 November 2015 06:44

0_87352.jpg


Ndugu zangu,
Nafuatilia kinachoendelea Zanzibar. Siioni namna nyingine ya kumaliza kadhia iliyotokea bali kwa pande mbili zinazokinzana kukubaliana kurudia uchaguzi. Walokosea wawajibishwe, lakini, hakuna namna nyingine yeyote ya kuhalalisha matokeo yatakayotangazwa baada ya uwepo wa kadhia, isipokuwa, kwa zoezi zima kurudiwa upya ikiwezekana chini ya uangalizi pia wa watu wa kutoka nje. Hivyo, kazi kubwa sasa na iwe kuyatafuta mariadhiano ili Zanzibar isonge mbele kutoka kwenye hali ya 'political impasse' iliyopo sasa.
Na ni heri kuyatafuta maridhiano kwanza kabla ya kuingia kwenye majadiliano, kuliko kuyatafuta maridhiano baada ya kuingia kwenye kugombana. Na MARIDHIANO ndio msingi wa UHALALI wa SULUHU itakayopatikana baina ya CUF na CCM.
Maana, tusipotanguliza busara, hekima na maslahi ya taifa, yumkini yaweza ikawa kama yale aliyopata kuyasema miaka 60 iliyopita, mwandishi yule mahiri, Mtanzania mwenzetu Shaaban Robert, aliandika; ” Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka wa matendo yetu mabaya ya zamani.
Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo.
Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote.”- Shaaban Bin Robert.
Na Mwanafalsafa Aristotle alipata kuandika, kuwa sifa kuu ya Ufalme ni Mamlaka, maana, Ufalme huwa ni sawa na Umungu Mtu. Ufalme huzaa despotism. Na HEKIMA ni sifa kuu ya Aristocracy, kwa maana ya tabaka la Uongozi . Naam, kiongozi sharti awe ni mtu mwenye hekima.
Na viongozi wanapokosa hekima wanaingia kwenye hali ya kuwa Ma-Oligarchy. Hiki ni kikundi kidogo cha wateule lakini waliojaa ubinafsi na choyo kubwa. Ni watu wasiojali maslahi ya umma bali ya kwao binafsi na kikundi chao.
Na sifa kuu ya Demokrasia ni ridhaa ya jamii. Naam, Demokrasia hujengwa katika msingi wa mariadhiano. Ikikosekana hali hiyo, ndipo makundi ya kuhasimiana huzaliwa, na hupelekea kuzaliwa kwa kinachoitwa ' mob tyranny', yaweza kusemwa uharamia au uongozi wa kimabavu wa kikundi fulani katika jamii.
Hivyo basi, Mwanafalsafa Aristotle anapendelea zaidi uwepo wa kinachoitwa ' Polity' aina ya utawala wa mchanganyiko. Utawala wenye kuhakikisha makundi yenye kuhasimiana yanapata fursa ya kugawana madaraka ili kuwepo na ' checks and balances'- kwamba kuwepo na hali ya kudhibitiana. Ndio msingi pia wa mgawanyo wa madaraka. Nchi lazima isonge mbele.
Maggid,
Dar es Salaam.
0754 678 252

Posted On Tuesday, 03 November 2015 03:13

Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu akizungumza na wafuasi wake wa chama cha AKChama cha AK cha Uturuki kimepata viti vingi vya bunge vitakavyoweza kudhibiti bunge la nchi hiyo baada ya kupoteza miezi mitano iliyopita.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa kwa siku kadhaa zijazo lakini karibu kura zote zimeshahesabiwa ambapo chama hicho cha AK kimejikusanyia zaidi ya asimilia hamsini kutawala bunge.

Matokeo hayo yatampa nguvu rais Recep Tayyip Erdogan ambaye aliita kura hiyo kama kura ya amani na ujumbe kwa wanamgambo wa kikurdi na kudai kuwa vurugu haziwezi kuishinda demokrasia.

Chama kinachoungwa mkono na Wakurdi cha HDP kimepata zaidi ya asilimia kumi zilizopigwa.

Katika eneo la kusini mwa mji wa Diyarbakir maafisa wa polisi walipambana na wafuasi wa chama hicho cha Kikurdi. Wandamanaji waliwatupia polisi mawe na mafataki huku polisi nao wakijibu kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Kufuatia ushindi wa chama chake cha AK Waziri mkuu wa nchi hiyo Ahmet Davutoglu alitoa hutuba ya kitamaduni katika makao makuu ya chama hicho mji Ankara. Davutoglu amesema chake kitaongoza kwa niaba ya Waturuki wote.BBC

Posted On Monday, 02 November 2015 03:53

Highness Kiwia akionyesha moja ya karatasi yenye makosa

Na:George Binagi-GB Pazzo

Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua kesia ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba haukuwa wa huru na haki kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.

Kiwia ambae ameshindwa kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa na Angelina Mabula kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na Uchaguzi huo.

Alieleza kuwa katika vituo mbalimbali jimboni humo kulikuwa na makosa mengi ambayo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kupigia kura pamoja na majina ya wapiga kura kukutwa katika majimbo tofauti na yale waliyojiandikishia.

Katika hatua nyingine Kiwia alikanusha taarifa kuwa alimtuma mwakilishi kwa ajili ya kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na kwamba siku ya kutangaza matokeo alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo kuzilai.

Kwa upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu linapaswa kulaaniwa kwa kuwa halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za uchaguzi.

Katika Matokeo ya Kiti cha Ubunge Jimboni Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina Mabula aliibuka mshindi baada ya kupata kura 85,424 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema Highness Kiwia aliepata kura 61,679 ambapo kwa upande wa Madiwani CCM ilishinda Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa na upinzani.

BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA

Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema.(P.T)

Posted On Saturday, 31 October 2015 04:11

Posted On Saturday, 31 October 2015 04:10

Republican

Trump alishutumiwa kwa mtazamo wake kuhusu wahamiaji

Wanaowania nafasi ya kuwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican walijibizana vikali kwenye mdhahalo wa tatu ulioandaliwa Colorado.

Donald Trump na Ben Carson, ambao hawana uzoefu mkubwa kisiasa lakini ndio wanaoongoza kinyang’anyiro hicho, walianza kushambuliwa tangu mwanzo wa mdahalo.

Gavana wa Ohio John Kasich alikashifu mpango wao “wa ndoto kuhusu ushuru” ana akaongeza kuwa: “Hatuwezi kumchagua mtu asiyeifahamu kazi.”

Bw Carson, ambaye ni daktari mstaafu, na ambaye amempita Bw Trump kwenye kura za maoni kitaifa, hakufana sana.

Pendekezo lake kuhusu ushuru, linalofuata mfumo wa zaka kwenye Biblia, ulishutumiwa vikali na Bw Kasich, ambaye pia alishutumu vikali mpango wa Bw Trump wa kufurusha wahamiaji 11 milioni kutoka Mexico na pia kujenga ukuta kwenye mpaka wa taifa hilo na Mexico.

Mdahalo huo haukujali urafiki wa kisiasa, kwani Gavana wa Florida Jeb Bush na Seneta wa Florida Marco Rubio pia walishambuliana.

Bw Bush alimhimiza Rubio, ambaye wakati mmoja alikuwa anajifunza siasa chini yake, kujiuzulu kutoka seneti kutokana na rekodi yake mbaya ya upigaji kura.

Wanahabari pia walishambuliwa, seneta wa Texas Ted Cruz akishangiliwa sana alipowashambulia waandalizi wa mdahalo huo CNBC kwa kuchochea uhasama.

"Maswali ambayo yameulizwa kwenye mjadala huu kufikia sasa yanayonyesha ni kwa nini raia huwa hawawaamini wanahabari," alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya chama cha Republican Reince Priebus pia alilalamikia maswali ya CNBC.

Upigaji kura wa kuamua wagombea urais utaanza Februari mwakani Iowa, miezi 10 kabla ya uchaguzi mkuu kufanywa.

Posted On Thursday, 29 October 2015 10:22

Stanslaus Shing'oma Mabula akiongea na wanahabari usiku wa kuamkia jana Octoba 27,2015 muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM) 

 BONYEA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA

Ezekiel Dibogo Wenje (Chadema) akiongea na wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa usiku wa Kuamkia jana.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jijini Mwanza ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo Titho Mahinya akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimboni Nyamagana.(P.T)

Posted On Thursday, 29 October 2015 03:35

nec

Jaji Damian Lubuva akiongea na wanahabari (hawapo pichani) leo.

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva hivi punde amesema kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar hakutasababisha kuahirishwa au kufutwa kwa uchaguzi wa Tanzania Bara na kusisitiza kuwa mchakato wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendelea kama ulivyopangwa.

Jaji Lubuva ameongeza kuwa tayari NEC imepokea taarifa zote za matokeo ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Zanzibar na hayakuwa na kasoro.

Aidha, Lubuva ameongeza kuwa uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unasimamiwa na NEC ambazo zina katiba mbili tofauti.(P.T)

Posted On Wednesday, 28 October 2015 16:41

uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi  Zanzibar, uliofanyika Oktoba 25, 2015.

Jecha amesema kuwa, ZEC imefuta matokeo ya uchaguzi kutokana na kukiukwa kwa sheria na taratibu mbalimbali za uchaguzi wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.

Uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku 90.

TAARIFA ZAIDI HAPA CHINI

Posted On Wednesday, 28 October 2015 16:38

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (katikati), akizungumza na mmoja kati ya vijana nane waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, kwa tuhuma za kusambaza matokeo ya kura za mgombea nafasi ya urais wa chama hicho katika mitandao ya kijamii kinyume na utaratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Imedaiwa vijana zaidi ya 190 walikamatwa kwa kosa hilo.

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam jana.

Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.

Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia.(P.T)

Posted On Wednesday, 28 October 2015 04:16

Mmoja wa wakazi wa Kijitonyama mpakani akipiga Kura yake

KITUO CHA KUPIGIA KURA NZASA

Posted On Sunday, 25 October 2015 17:08
Page 3 of 114

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu