We have 174 guests and no members online

WANANCHI katika majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini, watafanya uchaguzi wa wabunge wao kesho. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana.

Pia alisema wananchi wa Kata ya Mvomero mkoani Morogoro, nao watamchagua diwani. Wananchi wa maeneo hayo, hawakupiga kura katika uchaguzi mkuu, uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Siku hiyo, uchaguzi uliahirishwa katika majimbo saba, ikiwemo Arusha Mjini na Handeni Mjini, kata ya Mvomero na nyinginezo 34 nchini. Tangu wakati huo, uchaguzi umeshafanyika katika baadhi ya majimbo na kata.

Lubuva aliwaomba wananchi waliojiandikisha kama wapigakura katika majimbo na kata husika, kujitokeza kesho kwenye vituo walikojiandikisha ili kuweza kupiga kura na kuwachagua na viongozi wanaowataka.

IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

Posted On Saturday, 12 December 2015 08:03

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya Rais John Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa Arusha, Philemon Mollel (Monaban), uliofanyika katika kata ya Daraja Mbili jana, Kinana alisema sera ya kupambana na ufisadi ilizungumzwa katika kampeni na Dk Magufuli peke yake na si Lowassa wala kiongozi yeyote wa Ukawa.

Kinana alisema anamshangaa kiongozi huyo kwa kuwa mbali na kushindwa kuzungumza wakati wa kampeni za urais, pia hakuwa na hotuba yoyote ambayo ingeweza kukaririwa na Dk Magufuli.

Alisema Lowassa hakuweza kuzungumzia masuala yoyote ya kupambana na ufisadi kwa kuwa yeye ni mtuhumiwa na vyama vina vyounda umoja huo ndiyo vimekumbatia ufisadi kwa sasa.

Kwa mujibu wa Kinana, Lowassa alinadi sana mabadiliko kama angeweza kuingia madarakani, lakini hakufafanua ni mabadiliko yapi ambayo angeweza kuyaleta, wakati anatoka katika mfumo ule ule aliokulia kwa zaidi ya miaka 40 akiwa ndani ya CCM na Serikali yake.

“Jamani Lowassa alisema mabadiliko lakini hao wanaotaka mabadiliko wana umri wa ujana sawa na jua linalochomoza la saa mbili asubuhi, wakati yeye anayedai kuleta mabadiliko ana umri wa uzee sawa na jua linalozama la saa 12.30 jioni, si vichekesho hivyo?” Alihoji Kinana.

Alisema kutokana na ukweli huo, ndiyo maana Watanzania walipima na kuamua kumpa ushindi wa kishindo Dk Magufuli, kutokana na uadilifu wake pamoja na uwezo wake wa kuchapa kazi na kuamua kumnyima Lowassa na ndiyo maana kwa sasa anajifariji kwa kusema sera zinazotekelezwa ni za Ukawa.

Akizungumzia kazi alizoanza kuzifanya Rais Magufuli, Kinana alisema zimewakuna Watanzania wengi na kusema kuwa hiyo ndiyo kazi aliyoahidi kwao kuifanya na kwamba anaamini ataifanya kwa dhati katika kuwapigania wananchi wanyonge.

Mfumo CCM Akizungumzia madai kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayetokana na CCM anayeweza kupambana na machafu ndani ya Serikali, kwa kuwa hilo ni suala la mfumo, Kinana alipinga na kusema si kweli.(VICTOR)

Posted On Saturday, 12 December 2015 08:01

 

 

 

 

Posted On Saturday, 12 December 2015 03:36

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe A bass Ali Hassan Mwinyi, akitembelea Kituo cha Afya cha Fuoni Zanzibar kinachotowa huduma kwa Wananchi wa Jimbo hilo na jirani wakati akitimiza ahadi yake kwa kutuo hicha, akipata maelezo kutokwa kwa mdhamini wa kituo hicho Muuguzi wa Afya ya Jamii Bi Mwaka Pandu Makame akitowa maelezo ya eneo lao la kuchomea taka za kituo hicho.

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassan Mwinyi akitembelea kituo hicho cha Afya Fuoni Zanzibar akiwa katika ziara yake katika jimbo lake kujiuonea ufanisi wa kituo hicho na kukabidha Madawa na kuvifanyia mategenezo vyoo vya kituo hicho ni moja ya kero za Wananchi wanaofika kituoni hapo.(VICTOR)

Posted On Friday, 04 December 2015 09:58

Na Maelezo Zanzibar 30/11/2015

Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano.

Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla.

Amesema toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo.

“Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai.

Amesema kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa upya.

Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria.

“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai.

Katika taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema kuwaChama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri.

Vuai amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR(P.T)

Posted On Monday, 30 November 2015 15:28

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi ameimbia RFI Kiswahili kuwa, viongozi wa kisiasa kutoka serikali na upinzani wamekubaliana uchaguzi Mkuu kurudiwa tena.

Hata hivyo, Makamu huyo wa pili amedokeza kuwa hadi sasa haijaafikiwa ikiwa tume ya sasa ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Jecha Salim aliyefuta matokeo hayo itakubaliwa kusimamia uchaguzi mpya.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameeeleza kuwa rais Ali Mohamed Shein anaendelea kuwa uongozini kikatiba.Wananchi wa Zanzibar wanasubiri uamuzi wa viongozi wa kisiasa kuhusu mvutano huu wa kisiasa katka visiwa hivyo.

IMECHOTWA NA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

Posted On Friday, 27 November 2015 14:09

Mauricio Macri katika mji wa Buenos Aires Novemba 22, 2015.

Mauricio Macri katika mji wa Buenos Aires Novemba 22, 2015

Na RFI

Mauricio Macri kutoka chama cha Kiliberali amechaguliwa Jumapili hii kuwa rais wa Argentina katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais. uchaguzi ambao umeashiria mwisho wa utawala wa Kirchner alieliongoza taifa hilo la tatu kwa uchumi katika eneo la Amerika ya Kusini.

Tafiti angalau nne wa ziliofanywa na televisheni baada ya uchaguzi, zinampa ushindi Meya wa Buenos Aires. Matokeo ya kwanza rasmi yalikua yanatarajiwa kutangazwa saa 1:30 usiku saa za Argentina (sawa na 4:30 usiku saa za kimataifa).

Mauricio Macri, mwenye umri wa miaka 56, amemshinda Daniel Scioli, mgombea wa serikali ya mseto, ambaye alikuwa alipewa nafasi kubwa ya kushinda kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi.

Daniel Scioli akipiga kura katika kata ya Tigre, katika jimbo la Buenos Aires Novemba 22, 2015.

Rais Cristina Fernández de Kirchner kutoka chama cha mrengo wa kushoto, anaiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2007 baada ya kumrudilia mume wake, ambaye hakuweza kugombea awamu ya tatu mfululizo, kwa mujibu wa katiba.

Mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza, wafuasi wa meya wa Buenos Aires, walikutana katika makao makuu ya muungano wa vyama vya upinzani wa Cambiemos (ikimaanisha tubadili) unaongozwa na Macri, wamejipongeza na kuanza kusherehekea ushindi.

Wafuasi wa Mauricio Macri jijini Buenos Aires, Novemba 22, 2015.

Mauricio Macri atajitahidi kushirikiana na taasisi zingine za uongozi wa nchi kwa kuliongoza taifa hilo, kwani muungano wake hauna wingi wa viti katika Baraza la wawakili na Baraza la Seneti.(P.T)

Posted On Monday, 23 November 2015 04:43

Posted On Monday, 16 November 2015 04:24

Museveni

Juhudi za Mbabazi na Besigye kutaka kuafikiana mmoja wao ashindane na Museveni zimegonga mwambaRais wa Uganda Yoweri Museveni amesema wagombea urais wanaoshindana naye kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao si tishio kwake.

“Hiki hakitakuwa kinyang’anyiro kikali,” ameambia kikao cha wanahabari mjini Kampala.

Wapinzani wakuu wa Bw Museveni wanatarajiwa kuwa Amama Mbabazi na Kizza Besigye, ambao walikuwa marafiki wake wakuu wak

ati mmoja.

"Nasikia watu wakizungumza kuhusu kupiga vita ufisadi. Utawezaje kukabiliana na ufisadi ilhali twasikia ukiomba huyu na yule wajiunge nawe?” amesema.

"Lazima uwe na uwezo,” ameongeza Bw Museveni.

Hii ni mara ya kwanza kwa Bw Mbabazi, aliyekuwa waziri mkuu wakati mmoja, kuwania urais.

Bw Museveni ameongoza Uganda tangu 1986

Museveni

Museveni aliwasilisha karatasi za uteuzi kwa tume ya uchaguzi janaTume ya uchaguzi ya Uganda imeidhinisha watu wanane kuwania urais mwaka ujao wakiwemo Bw Museveni, Bw Besigye, Bw Mbabazi na Venansius Baryamureba.

Kampeni zitaanza Novemba. BBC

Posted On Thursday, 05 November 2015 05:15

TB Joshua

TB Joshua alimtembelea Rais Kikwete ikuluni Dar es Salaam

Mhubiri mashuhuri kutoka Nigeria TB Joshua ni miongoni mwa wageni mashuhuri watakaohudhuria sherehe ya kumuapisha John Pombe Magufuli kuwa rais mpya wa Tanzania Alhamisi.

Bw Joshua ambaye ni mhubiri wa kanisa la Church of All Nations aliwasili jijini Dar es Salaam Jumanne.

Baada ya kuwasili kwa mhubiri huyo, Bw Magufuli aliandika kwenye Twitter: "Tumushukuru Mungu, tumepata ugeni wa Nabii TB Joshua, atashiriki nasi katika sherehe nitakapoapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania."

Baadaye, alikutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ikulu ya Nairobi.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ambaye ni rafiki wa karibu wa Bw Magufuli, pia anatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo.

Tayari muungano wa Cord unaoongozwa na Bw Odinga umeahirisha shughuli ya kuwasilisha sahihi za kuunga mkono marekebisho ya katiba kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) ili kuhudhuria sherehe hiyo.

Muungano huo ulikuwa awali umepanga kuwasilisha sahihi hizo leo.

Bw Magufuli, aliyekuwa mgombea wa chama tawala cha CCM ataapishwa kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 25, matokeo ambayo yalipingwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema.

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Chadema Edward Lowaasa aliibuka wa pili, kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania.BBC

Posted On Wednesday, 04 November 2015 07:15

Kwenye Kutoelewana Mwanadamu Hawezi Kuikimbia Meza Ya Mazungumzo...
..Anaweza kuchelewa tu kuifikia...

Maggid.(P.T)

Posted On Tuesday, 03 November 2015 07:07

 

No. MBUNGE JIMBO CHAMA
1 Dk Charles Tizeba Buchosa CCM
2 Nimrod Mkono Butiama CCM
3 Omar Badwel Chilonwa CCM
4 Kanyasu John Geita Mjini CCM
5 Pudensiana Kikwembe Kavuu CCM
6 Sixtus Mapunda Mbinga Mjini CCM
7 Hassan Masala Nachingwea CCM
8 Abdallah Chikota Nanyamba CCM
9 Richard Mbogo Nsimbo CCM
10 Ester Matiko Tarime Mjini CHADEMA
11 Mwakajoka Frank Tunduma CHADEMA
12 Joshua Nassari Arumeru Magharibi CHADEMA
13 Dk Shukuru Kawambwa Bagamoyo CCM
14 Andrew Chenge Bariadi Magharibi CCM
15 Oscar Mukasa Biharamulo Magharibi CCM
16 Wilfred Lwakatare Bukoba Mjini CHADEMA
17 Jasson Rwikiza Bukoba Vijijini CCM
18 Dotto Biteko Bukombe CCM
19 Eshter Bulaya Bunda Mjini CHADEMA
20 Raphael Chegeni Busega CCM
21 Atupele Mwakibete Busekelo Rungwe Mashariki CCM
22 Bilango Samson Buyungu CHADEMA
23 Ridhiwani Kikwete Chalinze CCM
24 Anthony Mavunde Dodoma Mjini CCM
25 Freeman Mbowe Hai CHADEMA
26 Mboni Mhita Handeni CCM
27 Musa Ntimizi Igalula CCM
28 Dk Dalaly Kafumu Igunga CCM
29 Musa Hassan Zungu Ilala CCM
30 Janeth Mbene Ileje CCM
31 Anjelina Mabula Ilemela CCM
32 Mchungaji Peter Msigwa Iringa Mjini CHADEMA
33 William Lukuvi Isimani CCM
34 Njalu Daud Silanga Itilima Bariadi Mashariki Mkoa CCM
35 Jumanne Kishimba Kahama Mjini CCM
36 Josephat Kandege Kalambo CCM
37 Godfrey Mgimwa Kalenga CCM
38 Innocent Bashangwa Karagwe CCM
39 Silvestry Koka Kibaha Mjini CCM
40 John Mnyika (Chadema) Kibamba CHADEMA
41 Ally Seif Ungando Kibiti CCM
42 Hasna Mwilima Kigoma Kusini CCM
43 Kigua Omari Kilindi CCM
44 Vinance Mwamoto Kilolo CCM
45 Peter Lijualikali Kilombero CHADEMA
46 Vedasto Edger Kilwa Kaskazini CUF
47 Saidi Bungara Kilwa Kusini CUF
48 Luhaga Mpina Kisesa CCM
49 Suleman Nchambi Kishapu CCM
50 Emmanuel Papian Kiteto CCM
51 Edwin Sanda Kondoa Mjini CCM
52 Stephen Ngonyani Korogwe Vijijini CCM
53 Mary Chatanda Korogwe Mjini CCM
54 Shanif Mansoor Kwimba CCM
55 Dk Harrison Mwakyembe Kyela CCM
56 Innocent Bilakwate Kyerwa CCM
57 Zubery Kuchauka Liwale CUF
58 Onesmo ole Nangole Longido CHADEMA
59 Victor Mwambalaswa Lupa CCM
60 Cosato Chumi Mafinga Mjini CCM
61 Boniventura Destery Magu CCM
62 Dk Norman Sigala Makete CCM
63 Seif Gulamali Manonga CCM
64 Mashimba Ndaki Maswa Magharibi CCM
65 Stanslaus Nyongo Maswa Mashariki CCM
66 Mangungu Ali Mbagala CCM
67 Aroon Mulla Mbarali CCM
68 Joseph Mbilinyi Mbeya Mjini CHADEMA
69 Augustino Masele Mbogwe CCM
70 Zacharia Paul Isaay Mbulu CCM
71 Hassan Hassan Babali Mchinga CUF
72 Salum Khamis Meatu CCM
73 Joseph Haule Mikumi CHADEMA
74 Charles Kitwanga Misungwi CCM
75 Dustan Kitandula Mkinga CCM
76 Abdallah Ulega Mkuranga CCM
77 Rashidi Shangaz Mlalo CCM
78 Susana Kiwanga Mlimba CHADEMA
79 Julius Kalanga Monduli CHADEMA
80 Mgumba Omari Morogoro KusiniMashariki CCM
81 Anthony Komu Moshi Vijijini CHADEMA
82 George Lubeleje Mpwapwa CCM
83 Ezekiel Maige Msalala CCM
84 Nape Nnauye Mtama CCM
85 Livingstone Lusinde Mtera CCM
86 Hawa Ghasia Mtwara Vijijini CCM
87 Mahamoud Mgimwa Mufindi Kaskazini CCM
88 Mendrad Kigola Mufindi Kusini CCM
89 Atashasta Nditiye Muhambwe CCM
90 Rajab Adadi Muheza CCM
91 Charles Mwijage Muleba Kaskazini CCM
92 Pro Anna Tibaijuka Muleba Kusini CCM
93 Vedastus Mathayo Musoma Mjini CCM
94 Prof Sospeter Muhongo Musoma Vijijini CCM
95 Prof Jumanne Maghembe Mwanga CCM
96 Kangi Lugola Mwibara CCM
97 Dua Nkuruma Nanyumbu CCM
98 Cesil Mwambe Ndanda CHADEMA
99 George Mkuchika (CCM) Newala Mjini CCM
100 Alex Rafael Gashaza Ngara CCM
101 Joram Hongoli Njombe Kaskazini CCM
102 Ally Mohamedi Nkasi Kaskazini CCM
103 Desderius Mipata Nkasi Kusini CCM
104 Dk Diodorus Kamala Nkenge CCM
105 Stanslaus Mabula Nyamagana CCM
106 Hussein Kassu Nyangwale CCM
107 Hussein Bashe Nzega Mjini CCM
108 Jumaa Aweso Pangani CCM
109 Jenista Mhagama Peramiho CCM
110 Joseph Selasini (Chadema) Rombo CHADEMA
111 Mohamed Mchengerwa Rufiji CCM
112 Saul Amon Rungwe Magharibi CCM
113 Dk Mathayo David Same Magharibi CCM
114 Naghenjwa Kaboyoka Same Mashariki CHADEMA
115 William Ngereja Sengerema CCM
116 Steven Masele Shinyanga Mjini CCM
117 Joseph Kakunda Sikonge CCM
118 Tundu Lissu Singida Mashariki CHADEMA
119 Ahmed Salum Solwa CCM
120 Leonidas Gama Songea Mjini CCM
121 Aeshi Hilaly Sumbawanga Mjini CCM
122 Richard Ndasa Sumve CCM
123 Almas Maige Tabora Kaskazini CCM
124 Emmanuel Mwakasaka Tabora Mjini CCM
125 Abdallah Mtolea Temeke CUF
126 Ramo Makani Tunduru Kaskazini CCM
127 Daimu Mpakate Tunduru Kusini CCM
128 Saed Kubenea Ubungo CHADEMA
129 Joseph Mkundi Ukerewe CHADEMA
130 Waitara Mwita Ukonga CHADEMA
131 Magreth Sitta Urambo Mashariki CCM
132 James Mbatia Vunjo NCCR-Mageuzi
133 Japhet Hasunga Vwawa CCM
134 Gipson Ole Meseyeki Arumeru Magharibi CHADEMA
135 Joshua Nassari Arumeru Mashariki CHADEMA
136 Pauline Gekul Babati Mjini CHADEMA
137 Jitu Vrajlal Son Babati Vijijini CCM
138 Albert Obama Buhingwe CCM
139 January Makamba Bumbuli CCM
140 Boniphace Mwita Bunda Vijijini CCM
141 Lolesia Bukwimba Busanda CCM
142 Dr Merdad Kalemani Chananja Chato CCM
143 Juma Nkamia Chemba CCM
144 Ahmed Shabiby Gairo CCM
145 Joseph Musukuma Geita Vijijini CCM
146 Mary Nagu Hanang CCM
147 Magdalena Sakaya Kaliua CUF
148 Willy Qambalo Karatu CHADEMA
149 Daniel Nsanzugwanko Kasulu Mjini CCM
150 Holle Vuma Kasulu Vijijini CCM
151 Hamoud Jumaa Kibaha Vijijini CCM
152 George Simbachawene Kibakwe CCM
153 Peter Serukamba Kigoma Kaskazini CCM
154 Zitto Kabwe Kigoma Mjini ACT
155 Bawasili Mbaraka Kilosa Kati CCM
156 Suleiman Jaffo Kisarawe CCM
157 Dk Ashatu Kijaji KONDOA VIJINI CCM
158 Job Ndugai Kongwa CCM
159 Hassan Seleman Lindi Urban CCM
160 Kitwana Dau Mafia CCM
161 Dk Haji Mponda Malinyi CCM
162 Manase Njeza Mbeya Vijijini CCM
163 Martin Msuha Mbinga Rural CCM
164 Pascal Haonga Mbozi CHADEMA
165 Flatey Gregory Massay Mbulu Vijijini CCM
166 Mhandisi Kamwele Mlele CCM
167 David Silinde Momba CHADEMA
168 Mbena Joseph Morogoro Kusini CCM
169 AbdulaAziz Abood Morogoro Mjini CCM
170 Jaffar Michael Moshi Mjini CHADEMA
171 Sebastian Kapufi Mpanda Mjini CCM
172 Moshi Kakoso Mpanda vijijini CCM
173 Maftaah Nachuma Mtwara Mjini CUF
174 Suleiman Saddiq Murad Mvomero CCM
175 Rashid Akbal Newala Vijijini CCM
176 William Ole Nasha Ngorongoro CCM
177 Edward Mwalongo Njombe Urban CCM
178 Dr Khamis Kigwangalla (CCM) Nzega Vijijini CCM
179 Lameck Airo Rorya CCM
180 Kassim Majaliwa Ruangwa CCM
181 Marwa Ryoba Serengeti CHADEMA
182 Dk Godwin Mollel Siha CHADEMA
183 James Ole Millya Simanjiro CHADEMA
184 Philipo Mulugo Songwe CCM
185 Ahmad Katani Tandahimba CUF
186 Mussa Mbarouk Tanga Mjini CUF
187 John Heche Tarime Vijijini CHADEMA
Posted On Tuesday, 03 November 2015 06:46
Page 4 of 116

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu