We have 155 guests and no members online

Chopa aliyomo Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwasili kwenye Viwanja vya  Mulowo kuhutubia mkutano wa kampeni jana katika jimbo la Mbozi mkoani Mbeya, jana

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi  baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mlowo kuhutubia mkutano wa kampeni jana katika Viwanja vya Mlowo jimbo la Mbozi mkoani Mbeya. Pamoja naye ni Mjumbe wa katai ya kampeni za CCM Kitaifa Mwigulu chemba.

Wananchi wakiwa wamefurika Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni jana katika viwanja vya Mlowo jimbo la Mbozi mkoani Mbeya

Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni jana katika viwanja vya Mlowo jimbo la Mbozi mkoani Mbeya(P.T)

Posted On Monday, 19 October 2015 04:39

Posted On Monday, 19 October 2015 04:28

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Nghwira (kulia), na Mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chifu Litayosa Yemba wakijibu maswali mbalimbali katika mdahalo wa wagombea urais ulioandaliwa na Taasisi ya Twaweza Dar es Salaam leo. Hata hivyo wagembea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Magufuli na Edward Lowassa kupitia Chadema hawakuweza kuhudhuria kwa sababu mbalimbali.

 Waongozaji wa mdahalo huo wakiwa kazini. 

 Wadau wakiwa kwenye mdahalo huo.

 Raia wa kigeni na wadau wengine wakifuatilia mdahalo huo.(P.T)

Posted On Monday, 19 October 2015 04:05

 Bando la kumkaribisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan,likiwa limeshikwa na wananchi katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa  jana

 Chopa iliyomsafirisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa jana, ambako mgombea huyo alihutubia mkutano mkubwa wa kampeni.

 Chopa iliyomsafirisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa jana, ambako mgombea huyo alihutubia mkutano mkubwa wa kampeni.

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akipanda jukwaani baada ya kuwasili kwa Chopa, katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, kuhutubia mkutano wa mkutano  wa kampeni.

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia suluhu Hassan akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwa Chopa kuhutubia mkutano wa kampeni jana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga.(P.T)

Posted On Sunday, 18 October 2015 06:26

Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.

Dkt Shein emebainisha wazi kwenye mkutano huo wa kampeni kuwa Dkt Magufuli ni mtu sahihi na anatosha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano atashirikiana nae kwa kila jambo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua zaidi kimaendeleo.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.PICHA  ZOTE NA MICHUZI JR-KISIWANI UNGUJA.

Sehemu ya umati wa wakazi wa Kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo,ambapo Mgombea Urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufui aliwahutubia.

Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na kuwahutubia maelfu ya wakazi wa kisiwani Unguja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani humo.(P.T)

Posted On Saturday, 17 October 2015 04:28

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi 

Na Fredy Mgunda,Ismani

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi amembeza mgombea mwenzake anayegombea ubunge kwenye jimbo hilo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Patrick Olle Sosopi na kusema kuwa Sosopi hata afanye hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kauli ya Lukuvi aliitoa juzi wakati akiwahutubia wananchi wa vijiji vya Igingilanyi, Kising’a, Kinywang’anga, Mkungugu, Matembo na Ilambilole vilivyopo tarafa ya Isimani katika Jimo la Ismani alisema kuwa Sosopi hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa maana hana staha ya kuweza kuwashawishi wananchi kuwaletea maendeleo na badala yake anawabeza wagombea wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa kusema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 ya ubunge wa Lukuvi hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na chama hicho.

 “Mimi kiatu change navaa namba nane Sosopi anavaa namba moja hivi kweli ataweza kuwa mbunge wa jimbo hili?alihoji huku akishangiliwa sana na wananchi hao,kiukweli niwaambie kama mnataka maendeleo kichagueni CCM ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo na sio chama kingine.”alisema Lukuvi

Akiwa katika kijiji cha Kinywang’anga Lukuvi aliahidi kuwatafutia wananchi hao madaktari wa kutosha kwenye zahanati zilizopo kwenye jimbo hilo pamoja na dawa za kutosha ili kuendeleza huduma nzuri ya afya kwenye jimbo lake.

Alisma kuwa akatika kuendeleza kuduma nzuri ya afya tayari ameagiza gari ya kubebea wagonjwa(Ambulance) nchini Japani yenye gharama ya Tsh.mil 120 kwa ajili ya zahanati ya kijiji cha Kinywang’anga.

Alisema kuwa kwa sasa  tayari ujenziwa zahanati ya kisinga unaendelea na wanajenga wodi ya watoto,wodi ya wazazi pamoja na nyumba za kuishi watumishi ikiwa maendeleo yote yameletwa chini ya uongozi wa CCM.

Alisema kwa kipindi cha miaka miatano ijayo atahakikisha wananchi wake wanapata maji ya uhakika kutoka Jimbo la Iringa mjini ambayo yanatokana na Mto wa Ruaha.

“ Tayari fedha za kuvuta maji yam to Ruaha kutoka Iringa mjini hadi Ismani tumeshapata,wataalamu tayari wapo na wamesema muda wowote kuanzia sasa zoezi la maji Ismani litaanza”alisema Lukuvi

Aliongeza kuwa uongozi wa serikali ya magufuli hata kabla ya kuamua kugombea Urais tayari alishaweka mpango wa kutengeneza barabara ya Kising’a,Ilambilole,Mikongwi,Ngano hadi Ismani tarafani kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km.35 kwa gharama ya zaidi ya Uro milioni tano ambapo tayari ujenzi huo umeshaanza.

Wakati akihutubia wananchiwa kijiji cha mkungugu alisema kuwa atahakikisha atapandisha kiwango cha elimu kwenye jimbo hilo pamoja na kuweka haki sawa kwa wanawake na wanaume katika kumiliki ardhi.

Hata hivyo alisema kuwa suala la umeme kwenye jimbo hilo kwa baadhi ya maeneo ni la muhimu kwa sababu kuna maeneo yaliyopo ndani ndani hayana umeme hivyo atahakikisha ataleta nguzo kwa haraka ili wananchi hao waweze kuwa umeme.

“ Nitawapigania kuhakikisha umeme unaingia kwenye vijiji vilivyojificha sana ndani ndani na nawaambia lazima nitawaletea nguzo kwa maana mimi mwenyewe jambo la nguzo sitoshindwa.”alisema Lukuvi

Hata hivyo aliwataka wananchi hao kumchagua  mgombea urais wa CCM John Magufuli,mgombea ubunge Williamu Lukuvi pamoja na mgombea udiwani wa kata ya kising’a  Ritta Malagala ili waweze kuwaletea maendeleo ya jimbo hilo na sio mtu mwingine.

Alisema kuwa kwa uongozi wa Magufuli yeye hataki mchezo huu ni wakati wa kazi na sio lelemama na kama kutakuwa na kiongozi ambaye ataonesha amekaa legelege lazima atanyooka kwa maana magufuli hapendi mtu ambae sio mchapa kazi. (P.T)

Posted On Friday, 16 October 2015 05:55

Mgombe Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufulu akizumgumza na Wananchi na WanaCCM wa Kisiwani Pemba leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM zilizofanyika katika uwanja wa Gombani ya kale Wilkaya ya Chake chake Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wa Kisiwani Pemba leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli  katika uwanja wa Gombani ya kale Wilkaya ya Chake chake Pemba.

Maelfu ya wanaCCM waliofurika katika uwanja wa Gombani yakale Wilaya ya Chake chake Pemba wakimshangilia Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM kuomba Ridhaa ya kuchaguliwa katika nafasi ya kuiongoza Tanzania.

Maelfu ya wanaCCM waliofurika katika uwanja wa Gombani yakale Wilaya ya Chake chake Pemba wakimsikiliza Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akitoa sera za CCM leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM kuomba Ridhaa ya kuchaguliwa katika nafasi ya kuiongoza Tanzania.(P.T)

Posted On Friday, 16 October 2015 04:31

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Buseresere, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni jana

Vijana wa Buseresere, wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samaia Suluhu Hassan, msafara wake uliposimamishwa na vijana katika eneo hilo wakati akiwa  njiani kutoka Geita kwenda Bukoba mkoani Kagera jana

Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipozunguza na waliposimamisha msafara wake katika eneo la Buseresere, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni jana

Wananchi Buseresere

Mwana mama akiwa kazini wakati msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan aliposimamishwa na wananchi katika eneo la Buseresere mkoai Geita jana.(P.T)

Posted On Wednesday, 14 October 2015 06:35

MGOMBEA urais wa CCM, Dk John Magufuli amewataka wananchi kumchagua ili awe rais wa tano ajaye wa Tanzania huku akiahidi kushughulikia masuala mbalimbali ya wananchi na hivyo kuliletea Taifa maendeleo kwa muda wote atakaokuwepo madarakani.

Akizungumza na wananchi wa mkoani Lindi katika muendelezo wa kampeni zake, Dk Magufuli alisema akichaguliwa kushika nafasi hiyo, pamoja na mambo mengine atakayoyafanya atatumia utajiri wa gesi uliopo katika mikoa ya Kusini, kutoa ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ili kushusha bei na kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.

Amesema pia atatumia nafasi hiyo kutafuta namna bora ya kuwainua wakulima wa korosho, tofauti na utaratibu wa sasa wa stakabadhi ghalani, alisema umekuwa ukiwasababishia umasikini mkubwa wakulima wa zao hilo.

Akiwa Nachingwea, Ruangwa, Mtama na Lindi Mjini, Dk. Magufuli alisema tofauti na wapinzani wanaoahidi kuondoa nyumba za nyasi na tembe nchi nzima kwa siku 100 watakazokaa Ikulu, jambo alilosema ni ndoto, Serikali yake itakachofanya ni kushusha bei ya mabati, saruji, nondo, misumali na vifaa vingine vya ujenzi ili wananchi wajenge nyumba bora.

Akielezea ni vipi atawezesha hilo kufanikiwa, Dk Magufuli alisema atatumia utajiri wa rasilimali za Taifa ikiwemo gesi inayopatikanakatika Mikoa ya Kusini na Bagamoyo, Pwani ili kutoa ruzuku katika vifaa vya ujenzi.

Lakini, pia kuongeza viwanda vya bidhaa hizo ili kushusha bei kwa kiwango cha juu. Alisema dalili za kushuka kwa vifaa hivyo, zimeanza kuonekana baada ya kujengwa kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote mkoani Mtwara, ambachokinatumia nishati ya gesi kwa uzalishaji, kilichowezesha kushuka kwa bei ya saruji kutoka Sh 16,000 hadi Sh 8,000 na kwamba bei hiyo itashuka zaidi atakapokuwa rais.

Alisema pia ataziba mianya yote ya rushwa serikalini ili makusanyo ya fedha hizo yatumike kuboresha maisha ya Watanzania wakiwemo wa Kusini, huku akisema ushahidi wa utendaji wake kwa watu wa Kusini ni ujenzi wa barabara za lami kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara na baadaye Tunduru na Songea.

Ili kumwezesha kuingia Ikulu, mgombea huyo aliwaomba wakaziwa Mkoa wa Lindi kufika katika vituo vya kupiga kura mapema asubuhi ya Oktoba25, huku akisema kutokana na vitisho na vurugu zilizopangwa ili kuwatishia wananchi hasa wanawake wasipige kura, kutakuwa na polisi wa kutosha ili kulinda amani.

Akizungumzia soko la korosho, Dk Magufuli alisema akiingiaIkulu atabadili mfumo wa ununuzi wa korosho ili kuwezesha wakulima wa zao hilo kwa mikoa ya Kusini, kunufaika na kuboresha maisha yao na kuachana na mfumo wasasa ambao unawafanya wakulima kukopwa fedha zao bila kulipwa na hivyo kuwa masikini. (P.T)

Posted On Wednesday, 14 October 2015 03:42

Balozi Mwapachu Juma Volter

Balozi Mwapachu

TAMKO RASMI LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU

NAJIVUA UANACHAMA WA CCM

Ndugu zangu,

Leo ni siku muhimu katika kalenda ya Taifa letu. Tunamkumbuka marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetutoka miaka 16 iliyopita. Nadhani ni siku mwafaka kwangu kufanya maamuzi magumu katika maisha yangu ambayo yanahusu uanasiasa wangu. Mimi ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1967 wakati nilipojiunga na TANU Youth League. Nimepata fursa ya kuwa kiongozi ndani ya Chama hiki. Lakini kuanzia kesho mimi si mwanachama wa CCM tena. Natoa maelezo yafuatayo:

Kwa kipindi chapata mwezi na nusu hivi sasa mmekuwa mkisoma makala zangu kuhusu msimamo na mwelekeo wangu katika masuala ya siasa za hapa nchini hususan kuhusu uchaguzi mkuu na mstakabali wa demokrasia nchini mwetu. Nyote mnatambua kwamba kuanzia mchakato wa kumpata mgombe wa Urais ndani ya CCM kule Dodoma, ambako nilipiga kambi, sijayumba katika msimamo wangu kwamba Edward Ngoyai Lowassa ndiye chaguo langu katika kampeni za kumpata Rais mpya wa Taifa letu.

Chaguo langu si ndoto wala mlipuko wa mapenzi juu ya Lowassa. Nimemfahamu Lowassa tangu miaka ya 90 nikiwa cadre wa Chama cha Mapinduzi kwa mahusisho katika majukumu ya Kichama. Lowassa amejaaliwa nuru na uwezo wa kuongoza na wa kupendwa na watu. Ni msikivu pamoja na kwamba ni kiongozi asiyependa ukiritimba na utovu wa nidhamu, iwe kwa upande wa watumishi au wananchi wenyewe. Kubwa kwake ni ucha Mungu wake ambao unamsaidia sana katika uongozi unaojali na kuheshimu utu, ukweli na uwazi. Wanaodhani au kutaharuki kwamba eti anaweza au ana hulka ya kulipiza kisasi kwa jambo lolote lile ni waongo; wanajilinda.

Lowassa ni chaguo la wengi na CCM, katika busara yake ya kumuengua katika mchakato wa kumpata mgombea wa Urais, kimedhihirisha kutokuwa Chama kinachoendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Dalili za Chama hiki kupoteza lengo la kuwa Chama cha watu, na kuwa cha viongozi wachache zilianza siku nyingi na hasa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. CCM kimebadilika na kuwa Chama cha makundi na migawanyiko yakupambana, si kwa malengo ya itikadi na ujenzi wa Chama, bali ya kumalizana na kutaka kufukuzana.

Lowassa angeweza kufukuzwa miaka mingi tu iliyopita! Aliweza kushinda vita hivyo kutokana na kupendwa na wengi ndani ya CCM. Hivyo, kujitoa kwake uanachama wa CCM hivi karibuni ni sahihi kabisa kwasababu CCM si Chama tena cha watu. Kimetekwa. Na mimi nakubaliana na msimamo wa Lowassa na hao waliyofuata kutoka nadani ya CCM.

Niliwahi kuandika makala katika ukurasa huu nikimnukuu mshairi mmoja wa Uingereza aliyeandika kwamba, ‘there comes a time when the door opens and allows the future in’. Mlango huo sasa umefunguka usoni mwangu na huu uamuzi wangu maana yake ni kukubali kwamba wakati mpya umewadia; ni wakati wa mabadiliko. Kuendelea kujihisi kwamba ningali mwana CCM wa kadi ni kukubali kujidanganya mwenyewe. Si sawa. Kama marehemu Baba wa Taifa alivyowahi kusema, ‘CCM si mama yangu’.

Hivyo ndugu zangu, kuanzia kesho mimi si mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu kupitia ofisi ya CCM ya kata yangu Mikocheni, Dar-es-Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na Chama kingine.

Mwenyezi Mungu anilinde.(P.T)

Posted On Wednesday, 14 October 2015 03:34

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Ya Uchaguzi,
Waheshimiwa Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Msajili wa Vyama vya Siasa,
Viongozi wa Serikali,
Watendaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Demokrasia (DEP),
Watendaji wa Tume,
Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisheni wote katika Mkutano huu wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi pia kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.
Pamoja na kwamba mna majukumu mengi na ya muhimu mmetambua umuhimu wa mkutano wetu na mmekuja kuhudhuria mkutano huu kama ilivyotarajiwa. Tume imefarijika sana kukutana nanyi siku ya leo na tunawashukuru kwa moyo mliyoonyesha katika mchakato huu wa maandalizi ya Uchaguzi na wa kututhamini na kuja kuhudhuria Mkutano wetu.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Pamoja na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yenu kisiasa ni ukweli ulio dhahiri, kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa ni Wadau muhimu wa Uchaguzi ambapo mkishirikiana kutekeleza majukumu yenu kwa ufasaha mtaleta mafanikio katika uendeshaji wa Uchaguzi.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Vyama vya Siasa vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii, Tume inaamini kwamba ili Mpiga Kura aweze kufanya maamuzi sahihi ni muhimu kwake kupate Elimu sahihi. hivyo basi, Tume inatarajia kuona mkitumia majukwaa yenu vyema katika kuhamasishaji na kuelimishaji si tu wanachama wenu bali jamii nzima ya watanzania.(P.T)

Posted On Tuesday, 13 October 2015 03:57

magufuli akimnadi Nape katika jimbo la Mtamba viwanja vya soko la Majengo

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye katika Viwanja vya soko la Majengo

magufuli akimwaga sera katika viwanja vya mpilipili Lindi mjini

Magufuli akimwaga sera katika viwanja vya Mpilipili, Lindi Mjini.Magufuli akinadi sera katika jimbo la mtama viwanja vya soko la majengo

Magufuli akinadi sera katika jimbo la Mtama Viwanja vya Soko la Majengomagufuli na mama Salma Kikwete wakifurahia jambo

Magufuli na Mama Salma Kikwete wakifurahia jambo.(P.T)

Posted On Monday, 12 October 2015 19:18
Page 7 of 116

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu