We have 73 guests and no members online

Makundi Ya Waasi Drc Yazidi Kubanwa...!

Posted On Thursday, 29 November 2012 13:44 Written by
Rate this item
(0 votes)

Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, wakipiga kura kupitisha Azimio la kuongeza muda wa vikwazo vya silaha na vikwazo vinginevyo kwa makundi ya waasi yanayoendelea kuleta vurugu na machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mojawapo ya kundi la waasi linalobanwa na Azimio hilo ni lile la M23 ambalo hivi karibuni limetwaa mji wa Goma. Muda huo wa vikwanzo umeongezwa hadi februari Mosi 2014. Baraza hilo pia limesisitiza kwamba, mtu yoyote au taasisi inayojihusisha na kulisaidia kundi hilo la M23 kuacha mara moja la sivyo nao watakabiliwa na vikwazo vikiwamo vya kutosafiri na kusitishwa kwa mali zao.

 

Na: Mwandishi Maalum
Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa , limepitisha kwa kauli moja azimio linaloongeza muda wa vikwazo vya silaha na vikwazo vingine dhidi ya vikundi vya waasi ambavyo viko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Azimio hilo nambari 2078 ( 2012) linaelezea pia haja ya kuongeza vikwazo vya ziada kwa uongozi na wapiganaji wa kundi la waasi la M23, kundi ambalo hivi karibuni lilichukua Jimbo la Goma.
Baraza Kuu la Usalama ambalo lilikutana siku ya Jumatano limeongeza muda huo wa vikwazo hadi Februari Mosi mwaka 2014.


Vikwazo dhidi ya silaha viliwekwa kwa mara ya kwanza mwaka 2003 mara baada ya kumalizika kwa vita vya mara kwa mara nchini DRC, vita ambavyo vimedumu kwa miaka mitano na kukadiriwa kuua zaidi ya watu milioni tano.
Vikwazo vya silaha vimekwa dhidi ya makundi yenye silaha na ambayo si sehemu ya Jeshi la pamoja la Serikali au Polisi na pia vinahusu vikwazo ya kusafiri na usitishwaji wa mali za watu au taasisi ambazo zinakiuka vikwazo hivyo. Azimio hilo pia linalaani vikali kundi la waasi la M23, kundi ambalo linahusisha wanajeshi walioasi kutoka jeshi la kitaifa la DRC mwezi wa Aprili mwaka huu. Kundi ambalo kwa sasa linashikilia Goma, ambao ni Mji Mkuu wa Kivu ya Magharibi.


Baraza Kuu linalitaka kundi hilo la M23 na makundi mengine, kuacha mara moja aina zote za mapigano au vitendo vinavyosababisha uvunjifu wa amani. Aidha Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limeagiza na kurudia tena kusitishwa mara moja kwa misaada ya aina yoyote kutoka nje inayoelekezwa kwa kundi la M23. Kama hiyo haitoshi, Baraza Kuu la Usalama limeelezea nia yake ya kupanua wigo wa vikwazo siyo tu kwa viongozi wa M23 bali pia kwa yeyote yule ambayo kwa namna moja ama nyingine analisaidia kundi hilo la M23 au anakiuka vikwazo.
Wakati huo huo, Baraza Kuu la usalama pia limemwomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, kuliongezea muda Kikundi cha Wataalamu kuhusu DRC, hadi February Mosi mwaka 2014 ili kiweze kufuatilia utekelezaji wa vikwazo hivyo.


Katika hatua nyingine, Umoja wa Mataifa, umemtuma Mshauri wake Mkuu kuhusu masuala ya Kijeshi, Jeneral Babacar Gaye kwenda katika nchi za Maziwa Makuu ambako atakutana na kufanya majadiliano na wadau mbalimbali kuhusu masuala kadhaa yaliyojiri hivi karibu wakati wa mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu ( ICGLR).


Masuala hayo ni pamoja na utekelezaji wa kilomita 20 za Ukanda Huru ( Neutral Zone )eneo ambalo M23 litatakiwa kuondoka, na dhana ya kuwa na Jeshi la Kimataifa lisilofungamana na upande wowote.

( International Neutral Force).

Read 2579 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu