We have 198 guests and no members online

Ukitaka Kuijua Zanzibar Uyajue Na Mazonge Yake...

Posted On Sunday, 27 December 2015 02:51 Written by
Rate this item
(1 Vote)


.. Wanaosema Zanzibar haina Rais hawayajui mazonge ya Zanzibar, Kama Ingelikuwa Hivyo, Hata Mie Mwenyekiti Wetu Nisingetia Mguu Zanzibar...

Ndugu zangu,

Na nimepata kuandika hapa, ni vema tukakumbushana, kuwa historia ni Mwalimu Mzuri.

Wakati fulani mwaka 1984, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar walikutana pale Kisiwandui Imagechini ya Alhaj Aboud Jumbe, aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa JMT.

Ndani ya kikao kile walikuwamo wanasiasa wa aina ya Ramadhan Haji Fakhi, huyu alikuwa Waziri Kiongozi, alikuwamo pia Hamad Rashid, Hamis Shabaan Mloo, na Seif Sharif Hamad.

Wajumbe walizungumza jasho likiwatoka juu ya hali isiyo sawa kwenye Muungano yakiwemo madai kuwa Zanzibar haikuwa hata na fursa ya kukopa nje ya nchi kwa vile imo ndani ya Muungano.

Ikajengwa hoja ya Serikali Tatu. Wajumbe wote wakaafiki. Ikafika siku ya kuwasilisha hoja Dodoma.

Ajabu ya jambo lile, Julius Nyerere, alionekana kulijua hilo mapema sana. Alhaj Jumbe mkutanoni Dodoma akawa na wakati mgumu.

Wenzake wote akiwamo Seif Sharif Hamad waliikana hoja isipokuwa Ramadhan Haji Fakhi, Waziri Kiongozi.

Inasemwa, Julius Nyerere alimuuliza Ramadhan Haji Fakhi;
" Moja jumlisha moja ni ngapi?"
Jibu: " Tatu!"

Inasemwa pia, Julius Nyerere aliwachekesha wajumbe alipohoji ni shule gani aliyesoma Ramadhan Haji Fakhi yenye kufundisha hesabu kwa namna hiyo!

Hatma ya kikao kile cha Dodoma ni Alhaj Jumbe kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama ikiwamo kuachia Urais wa zanzibar. Ramadhan Haji Fakhi pia akunusurika, alikwenda na maji.

Ali Hassan Mwinyi akafanywa kuwa Rais wa Zanzibar na Seif Sharif Hamad akawa Waziri Kiongozi.

Mwaka mmoja na nusu baadae, mwaka 1985, Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano na akawa Rais kwa kuchaguliwa na Wananchi.

Inasemwa, kwa vile Ali Hassan Mwinyi alipata fursa hiyo, basi, Seif Sharif Hamad alitumaini angekuwa Rais wa Zanzibar.

Hapana, CCM ikamteua Idrissa Abdul Wakil kugombea nafasi ya Rais wa Zanzibar. Seif Sharif Hamad akawa ameukosa Urais na akafanywa kuwa Waziri Kiongozi. Kukawa na minong'ono ya Seif kulalamika chini chini.

Ikafika wakati kukawa na ' Hali ya Hewa ya kisiasa Iliyochafuka Visiwani'. Nilikuwa mwanafunzi pale Tambaza Sekondari. Ilinong'onwa mjini kuwa Rais wa Zanzibar, Abdul Wakil, kutokana na hali ya hewa kuchafuka, akawa anafanya kazi Unguja na anarudi kulala Dar es Salaam.

Siku moja wakati nikitoka shule na kupita maeneo ya Upanga kuelekea kituo cha mabasi cha Palm Beach, kwenye moja ya nyumba za eneo hilo, nikamwona kwa macho yangu Rais wa Zanzibar, Idrissa Abdul Wakil. Nikafahamu baadae, kuwa aliishi kwenye moja ya nyumba za eneo hilo.

Mwaka 1988, akina Seif Sharif Hamad , Hamad Rashid na wenzao, walitaka hoja ya Serikali Tatu ipelekwe tena Dodoma. Safari hii Idrissa Abdul Wakil aliipinga kutokana na uzoefu wa 1984.

Seif Sharif Hamad naye akaishia kupokonywa kadi yake ya uanachama CCM. Vuguvugu la mageuzi ya kisiasa duniani likaanza kwenye kipindi hicho. Lilitokea Ulaya Mashariki.

Ndipo akina Seif Sharif Hamad wakapata fursa ya kuanzisha KAMAHURU. Na baadae CUF ikaja pia. Na ndoto ya Seif Sharif Hamad ikabaki hai, ndoto ya siku moja kuwa Rais wa Visiwa vya Zanzibar.

Mwaka huu wa 2015, Seif Sharif Hamad amerusha tena karata yake. Anaweka rekodi, ya kuwa mgombea mkongwe kushinda wote, na mwenye uzoefu wa kugombea Urais kwa zaidi ya miaka 20. Kuna tunachojifunza.

Ndugu zangu Wajumbe,

Nimejaribu kukumbuka hayo. Nakaribisha maoni yenu pia...

Maggid,
Jambiani, Zanzibar.

MAONI YA WADAU KWENYE FB..

Lameck Mavipya · 3 mutual friends
Dah.....yataisha tu!
Like · Reply · 12 hrs
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · Friends with Ismail Jussa and 4 others
Haya tumeyaona na kuyatolea maoni siku nyingi.
Tulitaraji ungekikemea na kusikitishwa na yaliotokea ya ukwiukwaji wa katiba na Sheria ambayo yamesababisha haya leo. Unakwenda kutueleza ya miaka ya thamanini wakati haya ya leo ni makubwa kuliko haya.
U...See More
Like · Reply · 5 · 11 hrs
Abihud Greepherson
Abihud Greepherson · 13 mutual friends
Huyu majid ni mnazi wa ccm. Hoja zake nyingi ni za kinafiki
Like · Reply · 10 hrs
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · Friends with Freddy Macha and 4 others
Na yaangalie hayo uyaitayo mazonge ya Zanzibar yameanzia wapi?
Nitakuambia yalipoanzia, yalianza Tokea siku ya mtu yule ... Soma zaidi kwa kubofya hapo chini...

kutamka kwamba angalikuwa na uwezo angavichukua akaviweka mbaliiiii.
Like · Reply · 4 · 11 hrs
Kione Hamis Mahuruku
Kione Hamis Mahuruku Mwenyekiti napenda sana unavyojua kutukumbusha hasa sisi vijana tuliozaliwa miaka ya 80 ambao ndo Wahanga wakubwa wa siasa za sasa kutokana na ugumu wa maisha kuuhamishia ktk siasa! Jambo kubwa hapa ni kwamba,viongozi wengi wa siasa ni vigeugeu sana.Tunatakiwa tuwe makini sana.
Like · Reply · 3 · 11 hrs · Edited
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · 5 mutual friends
Haki za watu wa zanzibar kuchaguwa huitaki?maggid Mjengwa
Like · Reply · 11 hrs
Mohammed Ghassani
Mohammed Ghassani Mwenyekiti nadhani kuna data za kihistoria haikukaa sawa hapo. Kikao cha Kisiwandui na unachokitaka kiwe ushahidi wa Marehemu Mzee Idriss Abdulwakil kuhamia Bongo akikhofia usalama wake Unguja.
Like · Reply · 2 · 11 hrs
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · 5 mutual friends
Sijawahi kukusikia maggid ukisimama kwenye haki.
Like · Reply · 1 · 11 hrs
Hafidh Kido Jecha
Hafidh Kido Jecha Nassor je ulishawahi kumuona Seif Sharrif Hamad akisimama katika haki? Yeye si ndio alimkaanga Mzee Jumbe aonekane mbaya mpaka leo mwenzake yupo katika kizuizi cha nyumbani kwake. Halafu baada ya kukikosa alichoahidiwa anaramba matapishi yake. Wenzake wanaumia barabarani akipewa umakamu tu anatulia.
Unlike · Reply · 7 · 11 hrs
Juma Baraka
Juma Baraka Siasa za visiwani ni mazonge matupu kila siku unatakiwa uzitazame kwa jicho la 6
Unlike · Reply · 2 · 11 hrs
Shabani Amani Slim
Shabani Amani Slim · 11 mutual friends
Majjid ni msaka tonge,historia haiwez kumnyima mtu haki ya kuongoza kwa namna yoyote ile,hicho kigezo cha ccm kumuogopa Maalim kwa kisingizio cha mapinduz ni Ubazazi wa kiighuwana na ni ulaghai wa kuhalalisha udhalimu wao! Mwenyekit huwa anashadidia haya mambo kwa kigezo kilekile cha Ccm cha kusingizia mapinduz na muungano
Like · Reply · 3 · 11 hrs · Edited
Rashied Said
Rashied Said · Friends with Zitto Kabwe and 37 others
Ninacho jifunZa hapa, dhambi ya Maalim Seif kumsaliti mzee jumbe Ndio inayo Mnyima urais Leo
Unlike · Reply · 4 · 11 hrs
Vaginga Wa Vaginga
Vaginga Wa Vaginga · 15 mutual friends
Kwani ziara yako ilikuwa na uhusiano na rais!:-D:-D
Like · Reply · 11 hrs
Suleiman Shaaban Suleiman
Suleiman Shaaban Suleiman · 5 mutual friends
Hakuna sehemu iliyokuwa na siasa ngumu kama nchi ya Afrika ya Kusini na ndio nchi ya mwisho kupata uhuru kuliko zote na yaliisha hayo anayoandika Bw Maggid ni Nadharia inayotengenezwa kuhalilisha CCM kuendelea kubaki madarakani kama alivyofanywa Nelson...See More
Like · Reply · 3 · 11 hrs
Mshobozi Kamugisha
Mshobozi Kamugisha Burundi ina Rais: ninaomba tu mwenyekiti wote tukatae watawala wanaochezea ukarimu, uvumilivu, uungwana, na upendo wa amani wa Watanzania. Hivi vyote wanaotetea Dr Shein kuwepo madarakani hawavioni. Watanzania tumeamua kujitambulisha kwa hayo na tuheshimiwe
Like · Reply · 1 · 10 hrs
Suleiman Shaaban Suleiman
Suleiman Shaaban Suleiman · 5 mutual friends
Sawa kabisa Iwe tumechagua demokrasia iache iamue kupitia kura na sio hayo anayosema mtoa mada kuwa Zanzibar na mazonge yake.Sasa kama hilo la sasa limesababishwa na CUF au ni upande mmoja kutokubali kushindwa?...Kama anayofanya Nkurunzinza si sahihi basi iweje haya ya Shein na CCM yawe sahihi?
Like · Reply · 1 · 10 hrs
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · 5 mutual friends
Kiddo sijawahi nimewahi kukuona wewe!
Like · Reply · 10 hrs
Suleiman Shaaban Suleiman
Suleiman Shaaban Suleiman · 5 mutual friends
Hata Burundi inae Rais, Hata Compaore ni Rais Afrika ya Kati, Pia Kabila ni wa DRC sasa kwa melezo yake hakuna nchi isiyokiwa na mtawala iwe Rais, Mfalme, au hata Jeshi Swali Je yupo kikatiba na Sheria?....Hata kikwete alikiwepo tulikuwa na haja gani ya kufanya uchaguzi?
Like · Reply · 1 · 10 hrs
Abbas Salum Kitogo
Abbas Salum Kitogo Interesting!
Like · Reply · 10 hrs
Hafidh Kido Jecha
Hafidh Kido Jecha Nassor mimi si mwanaharakati, pia ni muumini wa kuona Zanzibar inatulia. Lkn Seif anatakiwa kutazamwa mara mbili. Amezungukwa na uroho wa madaraka. Mbinafsi na anataka yeye apate na si vinginevyo. Anao vijana damu changa kina Mansoor angeweza kuwatumia...See More
Like · Reply · 1 · 10 hrs
Mjd Salim
Mjd Salim · Friends with Mohammed Ghassani
Hafidh Kido Jecha Hilo lako liko wazi lakuegemea upande mmoja ambao una utashi nao kisiasa,Ukweli Maalim Wazanzibar Ndio wanaomtaka Na ndio chagua lao Na Ukweli kila Chaguzi anashinda kihalali lakini anadhulumiwa haki yake be transparent please.
Like · Reply · 10 hrs
Salum Hamad Ali
Salum Hamad Ali · 2 mutual friends
Ww unaupofu wa moyo huyo anaendelea kua Rais na wakati haumaruhusu tena yeye kua Rais tumwite nani? na bado Zanzibar haiko huru.
Like · Reply · 10 hrs
View more replies
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Ismail Zanga
Ismail Zanga Kumbe huyu Maalim Seif ni kama Lowasa anasaka urais kwa udi na uvumba miaka 20 yote yumo tu, kamsaliti mpaka mzee wa watu Jumbe, ni wakuogopwa kama ukoma Nyerere alisema.
Like · Reply · 1 · 10 hrs
Suleiman Shaaban Suleiman
Suleiman Shaaban Suleiman · 5 mutual friends
Hata Nelson Mandela aliusaka Urais kwa udi na uvumba
Like · Reply · 10 hrs
Ismail Zanga
Ismail Zanga Lakini hakusaliti wenzie, Mandela katumikia mda mdogo akakabidhi nchi lengo lake kuikomboa tu, wewe Mandela unamfananisha na huyo mroho wa madaraka, Mandela lini kajitangazia ushindi kabla kutangazwa? Jumbe na yeye wamekubaliana serekali 3 kampinduka baada ya muda na yeye anataka serekali 3 kuna aya kama sikosei 42 mungu anazungumzia wanafiki, hapati labda akhera kama kunauchaguzi.
Like · Reply · 9 hrs
Saraya Saraya
Saraya Saraya · Friends with Mohammed Ghassani
Mnasema alimsaliti jumbe, mlikuwepo kwenye hivyo vikao? Acheni upuuzi wa kushabikia dhulma ya kina shein
Like · Reply · 8 hrs
Ismail Zanga
Ismail Zanga Wewe ndio mpuuzi Saraya Saraya Hamad Rashid pia aliyesema na yeye alikuwepo kwenye kikao au ulikiwa bado uko mbwinde hujaja mjini.
Like · Reply · 7 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Huyo Hamad rashid kayasema Lini???
Like · Reply · 2 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Awe anasaka urais hata miaka 50 muhimu chama chake kimempitisha kikatiba na wananchi wanampa kura!!
Like · Reply · 1 hr
Maggid Mjengwa

Write a reply...

Choose File
Lino Thomasi
Lino Thomasi · Friends with Mussa Ally and 1 other
Like · Reply · 10 hrs
Khalilah Adaya
Khalilah Adaya · Friends with Mohammed Ghassani
Nafkiri hamuijui zanzibar naomba mkaulize tena historia yake kisha mje hapa kuropokwa
Like · Reply · 3 · 10 hrs
Mohamed Upunda
Mohamed Upunda · Friends with Mkubwa Kambi and 2 others
Hakuna kinachoweza kuhalalisha uhuni uliofanyika Zanzibar ule ni uhuni na wanaoutetea pia ni Wahuni
Like · Reply · 3 · 10 hrs
Makore Gabriel Musaroche
Makore Gabriel Musaroche Kumbuka Zanzibar inaongozwa na baraza la mapinduzi pia
Like · Reply · 10 hrs
Suleiman Shaaban Suleiman
Suleiman Shaaban Suleiman · 5 mutual friends
Baraza la Mapinduzi ni Jina tu ni sawa na Baraza la Mawaziri kwa huko bara.....ila sijui ulikuwa una maanisha nini?
Like · Reply · 10 hrs
Makore Gabriel Musaroche
Makore Gabriel Musaroche Baraza la mapinduzi sio jina tu ,hivyo ndo ukweli na historia ya Zanzibar kama haujui hivyo
Like · Reply · 9 hrs
View more replies
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Za'im Alrasady
Za'im Alrasady · Friends with Louis Kasuga and 1 other
Nimesoma mwanzo mwisho nlifkiri ntakuta kitu kipya kumbe ni yayo kwa yayo
Like · Reply · 1 · 10 hrs
Makore Gabriel Musaroche
Makore Gabriel Musaroche Tukumbuke Zanzibar ni nchi ya mapinduzi ndo maana wanasema mapinduzi daima!!!
Like · Reply · 10 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Sasa??
Like · Reply · 2 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Hebu nitajie aliepindua znz moja tu ambae yuko kwenye serikali sahivi?
Like · Reply · 1 hr
Shella Sa
Shella Sa · Friends with Abdallah Khamis
Ndio maana Maalimu kawafundisha nini mapinduzi mara hii,,,Kawapindua hata damu ya chawa haikumwagika
Like · Reply · 54 mins
Maggid Mjengwa

Write a reply...

Choose File
Seif Juma
Seif Juma · Friends with Mohammed Ghassani
Siasa ya Zanzibari ni kabla ya Mwaka 1964, kuanzia hapo tusidanfanyane hakuna siasa ya zanzibari, bali ni mazonge ya watanganyika kutaka kuitowesha zanzibari. Hilo la kwanza.
Lakini la pili mbona mnawasemea Seif na Jumbe mambo ambayo wao wenyewe wames...See More
Like · Reply · 3 · 9 hrs
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · Friends with Ismail Jussa and 4 others
Jecha ur comedian kwa sababu anaeshinda akanyimwa ushindi wake unasema ana uchu.waliong,ang,ania madaraka wako sawa?hawana uchu? Na kama Seif unasema angaliwe mara mbili una maana hata akishinda kwa Kura asipewe haki Yake ?
Like · Reply · 3 · 9 hrs
Maggid Mjengwa
Maggid Mjengwa Ndugu zangu, nimepata kusema, kuwa siasa za visiwani zina tofauti kubwa na bara. Kwenye kupigania uhuru wa Zanzibar kulikuwa na ASP iliyotokana na African Association na Shiraz Association. Kukawa na ZNP na ZPPP kwa maana ya Zanzibar Nationalist Party ...See More
Like · Reply · 1 · 9 hrs
Usia Nkhoma- Ledama
Usia Nkhoma- Ledama Kwanini iratibiwe ma ccm kama wazanzabari hawakuitaka ccm? Tunapiga kura za nini kama mratibu wa kudumu yupo? Tuache unafiki na kuharibiana sikukuu!
Like · Reply · 1 · 8 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Basi kuna ulazima gani wa kuwa na mfumo wa vyama vingi kwa Znz??
Like · Reply · 2 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Hizo ndio kasumba Zenu kua bila ccm znz haitokua salama yote wahafidhina na wasaka tonge Bado hawajesha kukinyonya kisiwa!
Like · Reply · 1 hr
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Ccm mwaka wa 51 huu wako madarakani mbona hiyo suluhu hatujaiona?? Zaidi YA kugawa watu Huyu mpemba Huyu muunguja Huyu mwarabu!
Like · Reply · 1 hr
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Ally Saleh
Ally Saleh Mwenyekiti umepotoka au unajipotosha makusudi...niko moja tu. Rais wa zanzibar anakuwa waziri aso wizara maalum na hadi leo hajaapishwa...viwaje?

Pili, kama yy rais mazungumzo mara 8 na maalim seif ya kazi gani?...See More
Like · Reply · 10 · 9 hrs
Wahbi Mohammed
Wahbi Mohammed · 2 mutual friends
Safi alberto
Like · Reply · 9 hrs
Saraya Saraya
Saraya Saraya · Friends with Mohammed Ghassani
Umenyooka ally saleh
Like · Reply · 8 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Hayo hawayaoni wao zaidi YA mapinduzi daima!
Like · Reply · 2 hrs
Maggid Mjengwa

Write a reply...

Choose File
Hafidh Kido Jecha
Hafidh Kido Jecha Nassor tunachojadili hapa ni maslahi mapana ya Zanzibar, kwa sababu ingawa sisi tunaishi bara lakini Zanzibar ni ndugu zetu. Kama ambavyo Mwenyekiti Maggid na familia yake leo hii wapo huko. Mnaniita ninaegemea upande mmoja, haya nyinyi wenye pande mbi...See More
Like · Reply · 9 hrs
Maggid Mjengwa
Maggid Mjengwa Ally Saleh, wewe unajua fika, kuwa wakati haujafika kwa unachodhania. Demokrasia katika nchi zetu ni mchakato. Tuliko ni kwenye hatua nyingine ya kimchakato. Tutafika unakotaka wewe na wengine, kimchakato na kwa kutanguliza maslahi mapana ya taifa letu, katika hilo usisahau kuwa jambo la visiwani ni letu bara, na kinyume chake.
Like · Reply · 1 · 9 hrs
Ally Saleh
Ally Saleh Hahaha...hatufiki kama na mara hii SMT itawasaliti au kuwatosa Wazanzibari wanaopiga kura.

Inafaa mjue kama wapiga kura sauti yao haiheshimiwe ni rahisi kushawishiwa kuingia ugaidi na wakichukua njia hii tanzania haitakua tena salama
Like · Reply · 2 · 9 hrs
Shamis Alkhatry
Shamis Alkhatry Sasa Majidd kama la Visiwani ni lenu pia hatujawahi kuwasikia Waandishi nyinyi wa upende wa pili kulivalia njuga na kuwaone huruma ndugu zenu hawa wa upande wa Pili ,kulaani hawa Mazombi wakiwavamia na kuwapiga Wazanzibari http://mwanahalisionline.com/mazombi-wahangaika-kuvamia-cuf/
Like · Reply · 9 hrs · Edited
Ally Saleh
Ally Saleh Mjengwa hajawahi na hana courage hio...hawezi kabisa kusimama upande wa haki zanzibar
Like · Reply · 9 hrs
Hafidh Kido Jecha
Hafidh Kido Jecha Shamis nami ni mwanahabari, na ukiangalia kwa umakini hiyo taarifa imeripotiwa na Mwanahalisi ambayo makazi yake ni Tanzania bara. Kuna vitendo vingi vya kihuni vinafanyika huku bara na vinaripotiwa kama ambavyo yanayofanyika Zanzibar yanaripotiwa.
Like · Reply · 9 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Ushawahi kukemea unyanyasaji wanao fanyiwa wananchi znz na mazombi?
Like · Reply · 2 hrs
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Salim Ferouz
Salim Ferouz Maggid Mjengwa Ahsante Kwa dondoo muhimu za Zanzibar, natamani mwanasiasa nnaemuona kuwa mmoja wa viongozi muhimu hapo baadae kwa Taifa letu kama angelisoma kidogo kutoka kwako kuhusu siasa za Zanzibar.Namzungumzia kiongozi wa chama kimoja kipya hapa nchini ambae amevalia njuga mambo ya Zanzibar badala us kuimarisha chama cake. Maoni yangu ni watu watulie waangalie uzoefu ulouelezea wa Maalim na viongozi wengine wa Zanzibar na kwa pamoja tuamini Zanzibar itabaki Salama.
Unlike · Reply · 2 · 9 hrs
Nassor Kharusi
Nassor Kharusi · 5 mutual friends
Nitasema tena Jecha kama ni jina lako halisi limekusibu. Kufanyika kwa vitendo hivyo bara havitoi fursa ya kuhalalika.
Like · Reply · 9 hrs
Khasim Omar
Khasim Omar · 3 mutual friends
Pigine porojo lenu la kiccm. Kina majidi mjengwa .lakini la ukweli ni kua 25/10/2015 walipiga kura na waliowengi walimchagua mtu wanaetaka awe rais wao.hizi nyengine ni mbwembwe tuu
Like · Reply · 1 · 9 hrs
Jamal Nassor
Jamal Nassor · 2 mutual friends
Khasim omar ww upo sawa kwani nani kwenye ccm alokua hajui nani kashinda ccm znz na ccm tanganyia lao moja ccm wa znz wao muhimu wavimbishe mifuko yao ccm tanganyia wao wanaendelea kua koloni lao ni Zanzibar hakuna jengine hizo zilobakia ni porojo tu lakini wafahamu vizazi vinavyo zaliwa muda huu watakuja kuchoka ndo watafahamu nn walicho kipanda hiyo ndo nasaha yangu
Like · Reply · 9 hrs
Said Ali
Said Ali · Friends with Maurice Mwanyika and 2 others
Hiyo picha mmoja anaonesha kulia na mmoja anaonesha kushoto wataelewana kweli hao.
Like · Reply · 9 hrs
Gamdad Murad
Gamdad Murad · Friends with Hashim Pondeza and 2 others
Kwann makala hizi zinaandikwa sasa hv wakati kuna utata Zanzibar?? Mwandishi amekusudia kuchochea utata na kuchafua amani ama vipi??
Like · Reply · 8 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Hawa Si ndio hao wasotutakia Kheir wanataka shari itokee Iki wazidi kutukandamiza ila in Shaa Allah Mungu hatosimama nao!
Like · Reply · 1 hr
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Kijani K Ali
Kijani K Ali · 2 mutual friends
Majjidi Maggid Mjengwa muongo na historia yako ya kisonge iyo
Like · Reply · 8 hrs
Soud Suleiman
Soud Suleiman · Friends with Nasib Faki
Naona mwamndishi anaongea ya nyuma ni kweli maalim alielemea kwengine kipindi hiko anachokiongea. Na ukweli kwamba jumbe alijikuta yupo peke yake. Binaadamu hukosea na na hasa unapokua kijana ila naamini kwamba yale ya nyuma sio ya saivi. Nia ya maalim...See More
Like · Reply · 1 · 8 hrs
Amour Khamis
Amour Khamis · 4 mutual friends
Maggid Mjengwa acha fitna yako na wacha kupotosha watu zungumza unachokijuwa
Like · Reply · 8 hrs
Amour Khamis
Amour Khamis · 4 mutual friends
History ya Zanzibar huijuwi wala hamutaijuwa kwa sababu hamutaki ukweli
Like · Reply · 8 hrs
Maggid Mjengwa
Maggid Mjengwa Amour, sawa, historia ya Zanzibar nayo ni siri, wengine hawapaswi kuijua!
Like · Reply · 8 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Ingekua vyema ungezungumzia na haki YA wazanZibar walonyanganywa na jecha 25 okt
Like · Reply · 1 hr
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Na unyanyasaji wanao fanyiwa wazanZibar na kikundi cha mazombi
Like · Reply · 1 hr
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Ali Khalifa Mohammed Al-Kharous
Ali Khalifa Mohammed Al-Kharous · Friends with Mohammed Ghassani
Sasa Siasa za Zanzibar zinakuhusuni nini!nyie tizameni macho hayakuhusu
Like · Reply · 8 hrs
Kijani K Ali
Kijani K Ali · 2 mutual friends
Maggid Mjengwa kumbe uko ovyo kiasi hiki
Like · Reply · 8 hrs
Soud Suleiman
Soud Suleiman · Friends with Nasib Faki
Jamani kuhusu hilo ni la ukweli kabisa. Hayo ni matunda ndani ya CCM na kuwagawanya waznz. Kufika mpaka ya kufika mpaka sasa ila watu wameamka na kuona kwamba sera za chama ni kua na upande mmoja hafifu na ukikubali hilo ndo mwanachama mzuri. Kiufupi ...See More
Like · Reply · 3 · 7 hrs
Mamaaisha Salum
Mamaaisha Salum · 7 mutual friends
Wao wameshika sefu wee sefu mbona hao walokua pamoja hawawataji? Na toka yatendeke hayo maalim stoke ccm mangapi yashafanyika YA kuiuza nchi bara hayo hayaonekani ila wajuwe usimuamshe alolala.......
Like · Reply · 1 hr
Maggid Mjengwa

Write a reply...
Choose File
Mokonzi Munene
Mokonzi Munene · Friends with Chaoga Tonge and 5 others
Maelezo yako mjegwa.... Tumesikia
Lkn Maalim hatafuti urais kwa njia haramu
Anautafuta urais kwa njia halali na wananchi ndio wametaka yeye awe rais ...See More
Like · Reply · 1 · 7 hrs
Suleiman Soud
Suleiman Soud · 2 mutual friends
Hana cha kuongea huyo majidi uccm umemzidi na chuki dhidi ya maalim lkn ataondoka yy maalim atamuacha mungu akipenda fisad mkubwa huyo
Like · Reply · 7 hrs
Abdalla Said
Abdalla Said · Friends with Daudi Ismail Isma
Muflis kama ni kukumbusha ya zamani wazee wakinya mwituni sasa watu wa sasa wanakunya ndani yaani self container.sasa unashauri watu warudi na tabia za kunya vichakani?
Like · Reply · 6 hrs
Issa Jumah
Issa Jumah Musimlumu saana unajua ukishakua ccm unakua hujui halafu hujui kama wewe hujui kwaivo unakua nimtu hatari sana
Like · Reply · 6 hrs
Exaveiry Simukuka
Exaveiry Simukuka Aise ilikuwa ucku wa giza!!
Like · Reply · 6 hrs
Salum Barkey
Salum Barkey · Friends with Wiz ẄêZẕý Ŝwåğğer
Wazanzibari wamepiga kura wamechaguwa viongozi wao kwa njia ya ki democracy kundi la wahuni wameleta dharau ya democracy ya wazanzibari na wewe unatuletea hadisi za alinache ni afadhali uandike wazi kama unaunga mkono uhuni ulofanyika kuliko kuleta story ambazo hazihusiani na mkwamo uliopo
Like · Reply · 5 hrs
Elias Peter
Elias Peter · Friends with Luqman Maloto and 5 others
Hii Historia yako fupi na tamu imenifurahisha sana sana 1+1=3.
Like · Reply · 1 hr · Edited
Imelda Mwasenga
Imelda Mwasenga · Friends with John Ulanga and 4 others
Mie napitatu namwachia Dr. Abdullah Makame afafanue
Like · Reply · 11 mins

Read 2809 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart