We have 389 guests and no members online

RAIS KABILA; “TUTAKUWA NA UCHAGUZI KAMA ULIVYOPANGWA”.

Posted On Saturday, 27 January 2018 10:03 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la joseph kabila

Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Kinshasa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, amesema anaiheshimu ratiba ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Rais huyo aliyoiongoza Congo tangu mwaka 2001, hakubainisha iwapo atawania tena nfasi ya Urais.

Pia ametumia mkutano huo kukanusha madai juu ya vikosi vya usalama, kwamba vinatumia nguvu kupita kiasi katika kusambaratisha maandamano ya amani yanayomtaka aondoke madarakani. Vile vile Kabila amelitaka kanisa Katoliki ambalo limekuwa likitekeleza maandamano ya kupinga utawala wake, kujihusisha zaidi masuala ya kidini ili kuepusha uvunjifu wa Amani. Kwa upande wa kanisa Katoliki ambalo bado mwafaka wake kisiasa tangu mwaka 2016 haujatekelezwa, limesema litaendelea kumshinikiza Kabila kuondoka.

Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa Mataifa, baada ya makabiliano kati ya waandamanaji na polisi Maandamano ya wiki iliyopita, yalisababisha vifio vya takribani watu sita.

Read 51 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli