We have 273 guests and no members online

RAILA ODINGA KUAPISHWA KESHO JUMANNE JAN.30 2018.

Posted On Monday, 29 January 2018 13:22 Written by
Rate this item
(0 votes)

   Picha inayohusiana

Kiongozi wa mungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Jamhuri ya Kenya Jumanne ya tarehe 30 January. Kuapishwa huko kunatokana na upinzani nchini Kenya kutokukubaliana na ushindi wa rais Uhuru Kenyatta aliyechaguliwa mwishoni mwa mwaka uliopita, ingawa upinzani haukushiriki duru ya pili ya uchaguzi baada ya matokeo ya uchaguzi wa awali kukataliwa na mahakama.

Hata hivyo baadi ya wafuasi wa NASA hawaungi mkono hatua hiyo. Pia wafuasi wa chama tawala cha Jubilee wanapinga vikali kuapishwa kwa Raila Odinga kwa kudai kuwa huenda machafuko yakatokea.

Tukio la kuapishwa kwa Odinga pia linapingwa vikali na Wakenya waishio nje ya nchi hiyo. Kwa upande wa jeshi la polisi nchini Kenya limeimarisha usalama mjini Nairobi katika eneo lililoteuliwa kwa ajili ya tukio hilo la kipekee, na kusisitiza kuwa hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kwenda eneo hilo, ingawa wafuasi wengine wa NASA wanaandaa usafiri wa kuelekea maeneo ya Nairobi kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa Odinga.

Read 102 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu