We have 280 guests and no members online

ZIFAHAMU BAADHI YA NCHI AMBAZO WAPINZANI WALIWAHI KUJIAPISHA.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 07:22 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la ODINGATokeo la picha la Etienne Tshisekedi.

 Hatua ya aina yake aliyochukua Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga kujiapisha kuwa rais wa watu wa Kenya sio ya kwanza kuchukuliwa na viongozi wa Afrika. Historia inazitaja baadhi ya nchi za Afrika ambazo viongozi wa upinzani waliwahi kujiapisha.

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO ETIENNE TSHISEKEDI.

Tokeo la picha la Etienne Tshisekedi.

Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko Zaire, na baadaye Laurent Kabila Joseph Kabila wa DRC

Mwezi Novemba 2011, Tshisekedi alijitosa kwenye kinyang'anyiro dhidi ya mtoto wa Laurent Kabila, kisha aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha katika uwanja wa Wahanga, Kinshasa kutibuka. Baadaye, aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani.

Ufanano kati ya Tshisekedi na Odinga ni kwamba wote wawili walikuwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka, wote walihudumu kama mawaziri wakuu na wote waligomea uchaguzi wa urais; Tshisekedi mwaka 2006, Odinga katika 2017.

NIGERIA MOSHOOD ABIOLA.

Tokeo la picha la , Moshood ABIOLA

Moshood Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa rais kipindi ambacho Rais Sani Abacha alipokuwa madarakani.

Hii ni baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi, kutafuta msaada ili kumkabili Abacha katika utawala wake.

Alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi ilipofika mwaka 1995, Siku aliyoachiwa kutoka gerezani, alikutana na ujumbe wa Marekani na kuhuduria mkutano.

Baada ya kupewa chai akiwa mkutanoni alianguka na kuzimia na hatimaye kufariki dunia.

GABON, JEAN PING.

Tokeo la picha la Jean Ping.

Mwaka 2016 Gabon, kiongozi wa upinzani Jean Ping alijitangaza mwenyewe kuwa rais na kutoa wito kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali Bongo ameshinda. Hata hivyo dunia nzima alijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo.

UGANDA KIZZA BASIGYE

Tokeo la picha la KIZZA BASIGYE

Kiongozi wa upinzani Nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za kula kiapo kuwa Rais wa Uganda baada yake kushindwa uchaguzini mwaka 2016 na Bw Museveni.

Chanzo,BBC.

Read 81 times

Add comment

Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu