We have 129 guests and no members online

KENYA; NYUMBA YA KIONGOZI WA UPINZANI YARUSHIWA GURUNETI.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 12:44 Written by
Rate this item
(0 votes)

Kalonzo Musyoka's home attacked

Ikiwa ni siku moja tu baada ya kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa rais wa watu nchini Kenya, kikosi cha kutegua mabomu kimetumwa katika nyumba ya kiongozi mkubwa wa upinzani nchini humo Kalonzo Musyoka baada ya kitu kilichodhaniwa kuwa ni bomu kurushwa katika eneo la nyumba yake jijini Nairobi.

Taarifa zilizoripotiwa katika gazeti la Daily Nation nchini humo zimesema shambulio hilo dhidi ya nyumba ya kiongozi huyo wa chama cha Wiper Democratic Movement (WDM) limekuja siku moja baada ya kushindwa kujitokeza katika sherehe yenye utata ambayo Raila Odinga alijiapisha kuwa rais wa wananchi. Mlinzi mmoja katika nyumba hiyo aliliambia jeshi la polisi kwamba watu waliokuwa katika magari mawili walipita katika nyumba hiyo na kufyatua risasi na kurusha kitu kilichoonekana kama guruneti katika eneo la nyumba ya Musyoka iliyopo eneo la Karen majira ya saa nane usiku.

Msemaji wa polisi wa eneo la Karen Cunningham Suiyanka ametibitisha kutokea kwa mkasa huo na kwamba hakuna taarifa za mtu kujeruhiwa

Read 54 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart