We have 135 guests and no members online

ALIYESIMAMIA KUJIAPISHA KWA ODINGA AKAMATWA.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 19:08 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la Tom Kajwang

Mbunge mmoja aliyefahamika kwa jina la Tom Kajwang ambaye pia ni wakili aliyesimamia zoezi la kujiapisha Raila Odinga amekamatwa na jeshi la polisi huku Serikali ikisema watu wengi watakamatwa.Wakili huyo ambaye ni mwanachama wa Muungano wa NASA alikamatwa na maafisa wa ujasusi alipokuwa mahakamani.

Waziri wa usalama Fred Matiang'i aliyesema hafla hiyo kuwa kinyume cha sheria amesema uchunguzi unaendelea na kwamba watu kadhaa watatiwa nguvuni. Hata hivyo hapajatolewa taarifa zozote kuhusu sababu za kumtia nguvuni. Zoezi la kuwakamata waliohusika katika zoezi la kuapishwa kwa Odinga limetangazwa na serikali ya nchi hiyo ingawa hakuna urasmi wa taarifa za kama Odinga naye atakamatwa. Wakati huo huo serikali imesema wakenya wataendelea kukosa kutizama vituo vitatu vya televisheni hadi uchunguzi utakapokamilika. Waziri Matiangi amedokeza kuwa sasa wanavichunguza vituo vya televisheni vya KTN, Nation Media Group pamoja na Citizen ambavyo amevitaja kuwa huenda vilikuwa na nia ya kushirikiana na wahalifu.

Read 76 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart