We have 151 guests and no members online

MWAKA MMOJA BAADA YA KIFO CHA KIONGOZI WA UPINZANI DRC, MWILI WAKE HAUJAZIKWA.

Posted On Thursday, 01 February 2018 14:46 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la Etienne Tshisekedi

 

Ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kifo cha aliyekua mpinzani mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi wa Mulumba, mwili wake unaelezwa kuwa bado haujarejeshwa nchini humo kwa minajili ya kuzikwa.Etienne Tshisekedi alifariki dunia Februari 1, 2017 nchini katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels. Kutokana na kukosekana kwa makubaliano kati ya chama cha UDPS na serikali mjini Kinshasa, mwili wa Tshisekedi bado umesalia katika chumba cha kuhifadhi maiti mjini Brussels.

Kwa upande wa kambi ya Tshisekedi mjini Brussels, kipaumbele cha kwanza ni kurejeshwa kwa mwili wa Waziri Mkuu wa zamani nchini DRC, ambako anapaswa kuzikwa, katika moja ya sehemu ya familia yake katika eneo la N'Sele, mjini Kinshasa. Familia ya kiongozi huyo tayari imelipa Euro 16,000 kwa ajili ya kuendelea kuhifadhiwa kwa mwili wa Tshisekedi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Brussels.

Kiongozi wa chama cha UDPS mjini Brussels, Mitch Katumba, amekua akikutana na viongozi wa Ubelgiji, Ufaransa pamoja na Ulaya, ili kuwezesha kurejeshwa kwa mwili wake nchini DRC. Mpaka sasa jambo hilo halijawezekana:

Bw Katumba amesema, "Kabila, haipaswi kuwa na hofu, sio mwili wa Tshisekedi ambao atamuondoa madarakani. hakuna hoja yoyote kwa Tshisekedi kuzikwa nje ya nchi, Tshisekedi atazikwa DRC, katika mji wa Kinshasa. Tutajitahidi kusafirisha mwili wake. Sisi ni Waafrika, na sisi ni watu kutoka jamii ya Bantu. Kuna desturi, tuna maadili yetu. Mjane hawezi kukaa hivyo kwa mwaka mzima, wakati ambapo hatujamzika mumewe ... Yuko hapo, analala chini, anaumia, ni mgonjwa, ".

Familia ya Tshisekedi inatarajiwa kushiriki katika maandalizi ya mazishi yaliyoandaliwa leo Alhamisi mchana mjini Brussels, kabla ya maombi yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika kanisa ya Brussels

Read 72 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu