We have 148 guests and no members online

“NAWAOMBA WASITISHE KAMPENI MWANASIASA HUYU AKIZIKWA WATAENDELEA” ZITTO KABWE.

Posted On Sunday, 04 February 2018 03:18 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for zitto kabwe msibani kwa kingunge

Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amevitaka vyama vya Chadema na CCM kusimamisha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani kwa siku tatu kama sehemu ya kuomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru. Akiwa kwenye msiba wa mwanasiasa huyo Kijitonyama, Zito amesema Kingunge alisaidia kuimarisha chama cha mapinduzi CCM na baadaye CHADEMA, hivyo sio busara vyama hivyo kuendelea na kampeni

badala ya kuomboleza kifo hicho. Katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro takribani vyama 12 vipo katika kampeni za ubunge zilizoanza Januari 21 na kutarajiwa kumalizika Februari 16 kabla ya uchaguzi kufanyika tarehe 17 mwezi Februari.

Kingunge alifariki dunia Februari 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na mwili wake unatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Read 64 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu