We have 149 guests and no members online

WANACHAMA WA ANC WAMTAKA RAIS ZUMA AJIUZULU.

Posted On Monday, 05 February 2018 07:03 Written by
Rate this item
(0 votes)

Related image

Kufuatia madai ya rushwa yanayomkabiuli Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na hivyo kusababisha wafuasi wengi kukihama chama tawala cha ANC nchini humo, maafisa wa juu wa chama hicho wamemtaka Rais Zuma ajiuzulu wadhifa wake. Katika mzungumzo maalum yaliyofanyika jana jumapili kati ya kingozi huyo na wanachama wake, wamemtaka achukue uamuzi huo ili kulinda heshima na hadhi ya Chama tawala.

Vile vile na jumatatu hii maafisa na wadau wenye ushawishi mkubwa katika chama cha ANC wanatarajia kufanya mkutano wa dharura ingawa haijafahamika ni hatua gani imepangwa kuchukuliwa katika mkutano huo. Lakini katika mkutano wa jana Jumapili karibu maafisa wote wa ANC walishiriki mkutano huo walionekana kuwa wamechoshwa na madai ya ufisadi yanayomkabili Zuma. Habari zaidi zaidi kutoka chama cha ANC zinasema vigogo wa chama wana wasi wasi kuwa hali hiyo ya ufisadi inaweza kukigawa chama endapo hakuna hatua itakayochukuliwa haraka iwezekanavyo kabla ya uchaguzi mkuu mwakani. Chama cha ANC kimepoteza umaarufu wake katika muhula wa pili wa Jacob Zuma, wakati ambapo mdororo wa uchumi unaendelea kushuhudiwa, huku Rais Zuma akiendelea kukabiliwa na tuhuma za rushwa.

Read 47 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu