We have 153 guests and no members online

AFYA YA KIONGOZI WA UPINZANI ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI IMERIPOTIWA KUWA KATIKA HALI MBAYA ZAIDI.

Posted On Tuesday, 06 February 2018 11:12 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for MORGAN TSVANGIRAI IN HOSPITAL

Hali ya Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai inaelezwa kuwa mbaya zaidi mapo mpaka sasa yuko katika hospitali moja nchini Afrika Kusini. Taarifa zilizotolewa na familia yake kwa vyombo vya habari zinasema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 ambaye anatibiwa saratani ya matumbo anakabiliwa na upungufu wa uzani , kuchoka na mishipa yake ya damu kua membamba. Tsvangirai ambaye ndiye kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe anafahamika zaidi kwa harakati zake dhidi ya aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe , na amepigwa na kufungwa jela mara kadhaa.

Image result for MORGAN TSVANGIRAI

Amekuwa akipelekwa hospitali mara kwa mara tangu mwezi Juni, akipokea tiba katika hospitali moja ya saratani mjini Johannesburg na baadae alirejea hospitalini humo mwezi uliopita.

Afya ya bwana Tsvangirai ilidhoofika kwa haraka siku ya Jumatatu , kulingana na duru za familia zilizozungumza na mtandao wa Bulawayo24 siku ya Jumanne.

Alipoteza hamu ya kula na akawa na tatizo kubwa la kula ama hata kumeza maji, duru zilisema.  Bwana Tsvangirai pia ameripotiwa kuwa na tatizo la kupumua.

Wakati huohuo Duru za MDC zimesema kuwa bwana Tsvangirai yuko hali mahututi na kwamba watu wanafaa kutarajia lolote lile.

Msemaji wa Tsvangirai Luke Tamborinyoka alisema kuwa kiongozi huyo wa MDC yuko hali nzuri lakini taifa linafaa kumuombea.

Hospitali ambayo bwana Tsvangirai anatibiwa haijatoa tamko lolote kuhusu swala hilo.

Read 74 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu