We have 158 guests and no members online

MGOMBEA WA UDIWANI AFIKISHWA DAR KWA MATIBABU

Posted On Thursday, 08 February 2018 15:01 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for Nelson Athanasio Makoti

Shughuli za kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Buhangaza wilayani muleba mkoa wa Kagera Mchungaji Nelson Athanasio Makoti zimesitishwa na Viongozi wa Chadema wilayani humo  ili kupata nafasi ya kushughulikia matibabu yake baada ya kuhamishwa Hospitali ya Kagondo hadi Dar es Salaam kwa matibabu. Katibu mwenezi wa Chadema Muleba Kusini, Hamisi Yusufu amesema hawezi kutaja alikolazwa mgombea huyo kwa sababu za kiusalama kutokana na hali ya upepo ulivyo kisiasa hapa nchini.

Amesema kampeni za uchaguzi wa udiwani Kata ya Buhangaza, zitaendelea kesho. "Suala la wapi mgombea amelazwa msemaji wake anaweza kuulizwa Tumaini Makene lakini kwa taarifa nilizopokea asubuhi ya leo ameonyesha mabadiliko tofauti na ilivyokuwa Kagondo," amesema Yusufu.

Hata hivyo, amesema wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu na kwa sasa Chadema hawaelekezi tuhuma zozote kwa kundi lolote la kisiasa. Amesema jukumu kubwa ni vyombo vya dola kufanya kazi ya kuchunguza na kubaini waliohusika kwa kusababisha mgombea kuathirika kiafya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Isack Msangi amesema katika mahojiano na Makoti na ndugu zake na wananchi hakuna mtuhumiwa anayeshikiliwa japo upelelezi unaendelea.

Read 49 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu