We have 157 guests and no members online

GEORGE WEAH AMTIMUA WAZIRI WA SHERIA

Posted On Friday, 09 February 2018 09:36 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for Charles Gibson OF LIBERIA

Rais mpya wa Liberia George Weah amemfuta kazi Waziri wa sheria Charles Gibson, baada ya malalamishi kuwa amepokonywa leseni ya uwakili baada ya kumtapeli mteja wake. Kabla ya uteuzi wake, Gibson alipatikana na hatia hiyo na Mahakama ya Juu baada ya kumtapeli mteja wake Dola za Marekani 25,000 na kuagizwa kuzirejesha.

Rais Weah amemteua Musa Dean aliyekuwa Wakili katika Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi hiyo. Mwanasoka huyo wa zamani wa Liberia alichaguliwa kuwa rais mteule ikiwa ni katika jaribio lake la pili toka awanie urais wa nchi hiyo.

Weah alichukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf ambaye alikuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuchaguliwa kidemokrasia ambaye alikabidhi madaraka kwa amani.

Rais Sirleaf alimshinda Weah katika uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika mwaka 2005, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo kadhaa nchini humo.

Read 69 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu