We have 156 guests and no members online

“HATUTAKUBALI…TUTAMLAZIMISHA KENYATTA KUHESHIMU KATIBA” MIGUNA MIGUNA.

Posted On Saturday, 10 February 2018 03:57 Written by
Rate this item
(0 votes)

Related image

Mwanasiasa na mwanaharakati wa Kenya Miguna Miguna ambaye alilazimishwa kwenda yuko uhami nchini Canada, alisema Ijumaa kwamba hataruhusu utawala wa rais Uhuru Kenyatta "kwendelea kutoheshimu sheria za Kenya."

Katika mahojiano ya moja kwa moja aliyofanya na shirika la habari la Marekani VOA, Miguna alisema kwamba mawakili wake tayari walikuwa wamewasilisha kesi katika mahakama moja mjini Nairobi kushinikiza serikali ya nchi hiyo kurejesha cheti chake cha kusafiria na vile vile kumruhusu kuingia nchini.

"Hatutakubali...Tutamlazimisha Uhuru kuheshimu katiba," alisema kwa njia ya simu kutoka nyumbani kwake mjini Richmond Hill, Ontario, Canada.

Aidha, Miguna alisema kwamba hatapumzika hadi pale serikali ya Uhuru Kenyatta itakapokubali kwamba haiko mamlakani kwa njia halali.

"Uhuru ni lazima aamue kama anataka kuongoza kwa mujibu wa katiba au la," alisema Miguna.

Alipoulizwa kama ana imani kwamba uamuzi utakaotolewa na mahakama juu ya suala hilo utaheshimiwa na serikali licha ya kutofanya hivyo hapo awali baada ya kuamriwa wawafikishe mahakamani watuhumiwa, Miguna, ambaye pia ni mwanasheria, alisema hawezi kulijibu swali hilo kwa sababu bado hatua hiyo haijafikiwa.

Alitaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike kabla ya mwezi Agosti. Miguna amesema kamwe hakuukana uraia wa Kenya na kwamba ana uraia pacha, ambao unnampa haki zote za raia wa nchi hizo mbili.

Kiongozi wa muungano wa National Super Alliance (NASA), Raila Odinga, alisema Jumatano kwamba angependa uchaguzi ufanyike mwezi Agosti. Miguna hata hivyo, alikuwa na maoni tofauti.

"Hata mwezi mmoja unatosha kufanya maageuzi ya mfumo wa uchaguzi yanayohitajika," alieleza Miguna.

Miguna aliwasili nchini Canada Jumatano usiku baada ya kuondoshwa kwa lazima nchini Kenya, ambako alikuwa anakabiliwa shtaka la uhaini.

Alisema kwamba atawasilisha malalamiko mengine kwenye mahakama kuhusu kuharibiwa kwa nyumba yake na maafisa wa polisi waliomkamata.

Kwa mujibu wa Miguna, maafisa waliokuwa na mavazi ya binafsi waliingia nyumbani kwake katika mtaa wa Runda wiki ilityopita na kutumia vilipuzi ili kumfikia kwenye chumba alimokuwa. Baadaye alipelekwa kwenye vituo kadhaa vya polisi na kufikishwa katika mahakama moja mjini Kajiado, takriban kilomita 80 kutoka mjini Nairobi, siku ya Jumanne.

Wakati wa mahojiao hayo, Miguna alisema kwamba licha ya kumkosoa vikali Raila Odinga na kusema kuwa hana uwezo wa kuiongoza Kenya, sasa amebadilisha msimamo.

Read 57 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu