We have 159 guests and no members online

KANISA KATOLIKI DRC LASEMA LITAENDELEA KUSHINIKIZA RAIS KABILA AJIUZULU.

Posted On Saturday, 10 February 2018 08:48 Written by
Rate this item
(0 votes)

Related image

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Viongozi wa Kanisa Katoliki wanasema, hawatachoka kuendelea kushinikiza kujiuzulu kwa rais Joseph Kabila. Mmoja wa viongozi wa Kanisa hilo Abbot Francois Luyeye amesema maandamano yataendelea kufanyika nchini humo katika siku zijazo.

Aidha, amesena kuwa Kanisa Katoliki linataka kuona DRC mpya na mabadiliko ya kisiasa nchini humo. Kanisa hilo lemye nguvu nchini DRC, linamtaka rais Kabila ajiuzulu na kutangaza kuwa hatawania urais mwezi Desemba mwaka huu. Rais Kabila ambaye muda wake wa kuendelea kuongoza kwa mujibu wa katiba umefika mwisho, hajasema iwapo atawania tena. Kabila aliingia madarakani mwaka 2001. Amelishtumu Kanisa Katoliki kwa uchochezi wa kisiasa kwa lengo la kuwasaidia wanasiasa wa upinzani.

 

Read 50 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu