We have 170 guests and no members online

MBIVU NA MBICHI KUHUSU ZUMA KUFAHAMIKA KESHO FEB 12.

Posted On Sunday, 11 February 2018 15:51 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for jacob zuma

Kamati kuu chama tawala nchini Afrika Kusini, imepanga kukutakuna siku ya Jumatatu kujadili hatima ya rais Jacob Zuma ambaye anashinikizwa kujizulu kwa madai ya ufisadi, madai ambayo ameyakanusha. Rais wa chama tawala cha ANC ambaye pia ni Naibu rais Cyril Ramaphosa amesema, raia wa Afrika Kusini wanataka suala hili kumalizika.


“Kamati kuu ya chama cha ANC itakutana kesho kujadili suala hili, kwa sababu watu wetu wanataka suala hili limalizike, kamati ya chama chetu itafanya hivyo,” alisema Jumapili.
Mkutano huo uliahirishwa wiki hii, baada ya kuwepo kwa ripoti kuwa kulikuwa na mazungumzo kati ya viongozi wa chama cha ANC n rais Zuma kuhusu uwezekano wa kuondoka kwake.
Ramaphosa alinukuliwa alikisema mazungumzo yalikuwa yanakwenda vizuri na mwafaka huenda ukafikiwa hivi karibuni.
 Hata hivyo, rais Zuma ameendelea kukataa madai dhidi yake na kusema hakufanya kosa lolote na chama kinaweza kufanya lolote linalotaka ikiwa ni pamoja na kumwagiza aachane na urais. Kumekua na maandamano kwa miezi kadhaa kumshinikiza Zuma ambaye amekuwa rais tangu mwaka 2009, kujiuzulu.

Read 74 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu