simulizi

Simulizi Za Kusisimua: Evertons Waligombana Wao Kwa Wao Ikazaliwa Liverpool FC 1892!

on

Ndugu zangu, Si wengi wenye kufahamu chimbuko la Liverpool FC kama klabu. Liverpool FC iliundwa Machi 15, 1892 kufuatia ugomvi wa kugombania uwanja wa Anfield.

Rais wa Evertons wakati huo, Bw. John Houlding aliununua kwa fedha zake uwanja wa Anfield mwaka 1891, baadae akaingia kwenye ugomvi na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya timu.

Wajumbe wa Bodi waliotofautiana na Rais wao wakaamua kuhama na timu yao ya Evertons kuhamia uwanja wa Goodison Park.

Pale Anfield akaachwa Rais wa klabu John Houlding bila timu!

Houlding akaitisha kikao cha dharura nyumbani kwake Anfield Road. Wajumbe walioudhuria kikao hicho chini ya John Houlding wakaazimia kuanzisha klabu mpya ya Liverpool FC.

Simulizi hii kwa hapa nyumbani inafanana na ugomvi wa Yanga uliozaa Pan African na ugomvi wa Simba uliozaa Red Star. Na ajabu ya ugomvi uliozaa Red Star ni babu yake Haji Manara, nadhani aliitwa Hassan Haji, alikuwa kiongozi wa Simba na ambaye Simba walimtuhumu yeye na baadhi ya wenzake kuhujumu timu.

Wakati huo Simba ilikuwa ikipoteza mechi kwa Yanga na mchezaji wa Yanga, Sunday Manara, mkwewe alikuwa Mzee Hassan Haji, babu yake Haji Manara! Hivyo, tuhuma za viongozi wa Simba kwa kiongozi mwenzao, zilikuwa zinaelekezwa ukweni!

Turudi kwenye simulizi mama.
Ishara zote zinaonyesha Simba watawafunga Gor Mahia na hivyo kwenda Uingereza, kupambana na Evertons ambayo kihistoria ni timu iliyohama uwanja na kupelekea kuundwa kwa Liverpool FC!

Maggid.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *