michezo

Sir Alex Ferguson Afanyiwa Upasuaji Kwenye Ubongo Wake.

on

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson jana Mei 05, 2018 amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye kichwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Manchester United, imeelezwa kuwa upasuaji huo unahusisha ubongo na umeenda vyema lakini anahitaji muda wa uangalizi wa makini zaidi.

Kufuatia hali hiyo, Mtoto wa Sir Alex aitwaye Darren Ferguson ambaye pia ni kocha wa klabu ya Doncaster jana alishindwa kuhudhuria mechi kati ya klabu yake dhidi ya Wigan.

Baadhi ya wachezaji wametoa pole kwa familia ya mzee Ferguson kufuatia taarifa akiwemo Robin Van Persie,  Diego Forlan na wengineo.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *