habari

Sudan Kusini Kuanza Mazungumzo Ya Amani.

on

Mazungumzo ya amani nchini Sudan Kusini yanaanza tena katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Abba, yanayolenga kufikia amani ya kudumu na makubaliano ya kuachiliwa kwa aliye kuwa makamu wa rais Riek Machar, ambaye yuko katika kizuizi cha nyumbani nchini Afrika Kusini.

Mazungumzo hayo yanaanza wakati ambapo makundi mapya ya waasi yanaendelea kuundwa, kwani hivi karibuni aliyekuwa Mkuu wa Majeshi nchini humo, naye ameunda jipya kundi la waasi.

Paul Malong ambaye alitimuliwa katika wadhifa wake na Rais Salva Kiir mwaka uliyopita, amechukua hatua hiyo dhidi ya utawala wa Kiir.

Malong ambaye amekuwa akiituhumu serikali kwa rushwa na makosa yamengine ya ufisadi, amesema kuwa kundi lake litakuwa na jukumu kubwa la kuiondoa Sudan Kusini kwenye sintofahamu na kuielekeza katika demokrasia na maendeleo.

Malong alituhumiwa mara kadhaa na Umoja wa mataifa kwa kuratibu mashambulizi ya kikabila dhidi ya raia. Sudan Kusini imeendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita hivyo vilianza mwaka mmoja tu baada ya taifa hilo changa kujipatia uhuru wake.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *