siasa

Sugu Na Masonga Waachiwa Huru.

on

Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Joseph Mbilinyi (Sugu) na Katibu wa CHADEMA Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga, wameachiwa huru baada ya kumaliza kutumikia kifungo cha miezi mitano jela.

Sugu na Masonga Walifungwa katika Gereza la Ruanda Jijini Mbeya baada ya kukutwa na hatia ya Uchochezi.

Hukumu hiyo ilitolewa Februari 26 mwaka huu jijini Meya na walishtakiwa kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi katika mkutano wa hadhara.

Saa chache baada ya kutoka jela Joseph Mbilinyi aliongea na MCL Didital na kusema kwamba ni mfungwa wa kisiasa, na kwamba alifungwa kiholela na ametoka kiholela.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *