habari

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Uteuzi Wa Wajumbe Wa Bodi Ya Wakurugenzi Wa Shirika La Kuhudumiaviwanda Vidogo (SIDO)

on

Kufuatia Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumteua Prof. Elifas Tozo Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya SIDO, Mheshimiwa Joseph George Kakunda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, kwa Mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Ibara ya 1(b) ya Jedwali la Sheria ya SIDO ya mwaka 1973, amewateua Wajumbe sita (6) wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).
Wajumbe hao walioteuliwa ni:-
  1. Bw. Maduka Paul Kessy (Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma);
  2.  Prof. Bashira Alli Majaja (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam);
  3.  Bi. Seraphia Robert Mgembe (Mratibu wa MKURABITA);
  4. Mhandisi Peter Daud Chisawilo (Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Intermech Engineering Ltd na Mhandisi Mkuu Mstaafu wa Shirika la Mzinga);
  5. Bw. John Mihayo Cheyo (Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais TAMISEMI); na
  6.  Mhandisi Gilman Kasiga (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Kimataifa ya General Electric – GE).
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 3 Februari 2019.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *