habari

Taarifa Ya Basi Kugonga Treni Ya Mizigo Na Kusababisha Vifo-Kigoma.

on

Watu saba wameripotiwa kufariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Princess Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD linalotoka Kigoma kwenda Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora, kugonga treni ya mizigo eneo la Kahabwa Kata ya Gungu mkoani Kigoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Jumatano hii, Juni 6, 2018 majira ya saa 12:15 asubuhi, baada ya basi hilo kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi hilo.
Dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa waliofariki dunia, huku idadi ya vifo ikisemekana inaweza kuongezeka kutokana na hali mbaya za majeruhi.

Kamanda Otieno amesema jeshi lake linaendelea kushughulikia ajali hiyo na kwamba taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *