siasa

Taarifa Ya Mbunge Wa Monduli (CHADEMA) Kujiunga na CCM.

on

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Mhe. Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM muda huu kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi rais Magufuli.

“Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa… Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu… Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi,” amesema Julius Kalanga Laizer ambaye amepokelewa na katibu mwenezi wa CCM ¬†Humphrey Polepole.
Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema 2015.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *